Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ushindi wa Faye na upinzani nchini.. kuna lakujifunza?

Faye Sds Ushindi wa Faye na upinzani nchini.. kuna lakujifunza?

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mara ya kwanza katika chaguzi kumi na mbili za urais zilizofanyika chini ya sheria ya upigaji kura wa watu wote tangu Senegal ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, ambapo mgombea wa upinzani ameshinda katika duru ya kwanza ya upigaji wa kura.

Mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye (44) ambaye ni wachache waliokuwa wakimfahamu chini ya mwaka mmoja uliopita zaidi kwa waliokuwa nje ya chama chake cha Pastef, anajiandaa kuchukua kiti Ikulu kitakachoachwa wazi na Mack Sall aliyemaliza vipindi vyake viwili ikulu.

Kama ilivyo kwa wapinzani wengi wa Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania, Bassirou Diomaye Faye na mshirika wake wa karibu Ousmane Sonko, wanayo mifululizo ya hadithi za kufanana na zenye vionjo vya kuwakatisha tamaa na kuwaweka katika majuto ya kisiasa.

Wote wamekiri mara kadhaa kukumbana na kashkash za polisi, kesi za kutunga, kupishana rumande mara nyingi na hata kulala jela mara nyingi na vyama vyao kuwa katikati ya mitego mingi na uhuru mdogo uliokandamizwa na kutegeshwa miiba mingi inayotokana na amri nyingi batili kutoka kwa mamlaka,upendeleo wa dola na sheria nyingi kandamizi na zenye upendeleo mkubwa kwa chama tawala.

Kwa Bwana Faye na Sonko kwao wao baada ya miezi kadhaa ya jela wote wawili kwa pamoja, waliachiliwa huru wiki moja tu kabla ya uchaguzi mkuu na hilo halijawazuia kuwabwaga washindani wao waliokuwa na muda mrefu wa kufanya kampeni uraiani akiwemo waziri mkuu wa zamani na mchumi Amadou Ba.

Wawili hao pia walikuwa na chama cha siasa kiitwacho Pastef, chama ambacho kilifutwa baadae na mamlaka za Senegal kwa mashtaka kadhaa ambayo wawili hao wanaamini kuwa yalikuwa mashtaka ya kutunga ili kuwadhohofisha na kuwatoa kwenye ramani ya siasa za Senegal.

Tayari tume ya uchaguzi nchini humo imesema matokeo ya awali yanaonesha kuwa Bwana Faye ana karibu asilimia 53.7 ya kura zote na Amadou Ba akiwa na asilimia 36.2 kwa kuzingatia hesabu kutoka asilimia 90 ya vituo vya kupigia kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Matokeo ya jumla yanatajiwa mwishoni mwa wiki hii.

Ili kushinda urais nchini humo na kuepuka duru ya pili ya uchaguzi mshindi anataliwa walau kuwa na kura zaidi ya asilimia 51.

Wakati huu kunashuhudiwa msururu wa salamu za pongezi zinazoonekana kuwa nyingi mitandaoni hasa zile za kutokea kwa vyama na wanasiasa wa upinzani barani Afrika, salamu hizo zimebebwa na imani na matumaini makubwa kuwa Bwana Faye amefungua njia yenye mwanga wa matumaini kwa vijana wanasiasa na vyama vya upinzani barani Afrika.

Lipo la kujifunza Senegal?

Kuna utofauti gani wa kisiasa kati ya "wale wa Senegal na hawa wa kwetu?"

Columnist: www.tanzaniaweb.live