Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Unafahamu wadudu unawabeba mdomoni wakati wa kubusu?

Kissing Bakteria wengi wanaingia mdomoni kupitia kubusu, tunawameza.

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: BBC

Busu linaweza kuwa kitu kizuri kwenye mapenzi, lakini unajua ukimbusu mwenzi wako, nini unachokitoa?

Wakati mwingine watu huchukuliwa kawaida kwamba tunadhani tunaongeza upendo na kushirikiana kwa upendo, lakini kuna jambo ambalo labda hatutambuiā€¦ kwa kumpiga busu mwenzi wake fahamu mnasambaziana vijidudu vingi!

Ingawa inaweza isionekane hivyo, lakini mfumo wa kinywa ni tata na unaweza kuhifadhi hadi aina 700 za bakteria wanaoweza kuishi. Kwa namna mfumo wa kinywa ulivyo unawezesha mate kutengeneza unyevunyevu wenye joto la wastani lakini pia muda wote unawezesha usambazaji wa virutubisho. kwa hivyo hali hii inasaidia kwa bakteria kuzaliana na kukua.

Kwa kuwa mdomo umejaa vijidudu, ni dhahiri kwamba tunaweza kupeana vijidudu hivi wakati tunabusu.

Ukweli ni kwamba, kwa mujibu wa utafiti mmoja uliofanywa na wanafunzi nchini Uholanzi, unabainisha kwamba ukimbusu mtu kwa sekunde 10 tu jua mnaweza kuhamishiana baina yenu bakteria wengi wanaofikia milioni 80.

Je ni vijidudu gani huingia mdomoni mwako? Jamii ya bakteria waliopo mdomoni inajulikana kama 'microbiota' ambao huwepo tangu kuzaliwa. Hubadilika kulingana na kile tunachokula, kama ni dawa au la, usafi wetu au ikiwa tunavuta sigara. Umri na maumbile ya mtu pia huathiri muundo wa 'microbiota' hawa. Pamoja na hayo kwa ujumla, bakteria wanaoishi kinywani mwa binadamu huwa na faida nyingi. Kubwa husaidia kuzuia utengenezwaji wa vimelea vya magonjwa, husaidia kinga ya mwili na mfumo wa kumengenya pamoja na kudhibiti shinikizo la damu.

Bakteria waliopo mdomoni, tunakua nao tangu utoto. Bakteria hawa wanaishi katika jamii na kwenye sehemu tofauti za mdomo, na hutengeneza 'biofilms'. Hujibanza kwenye kuta za maeneo mbalimbali ndani ya mdomo hasa kwenye 'substrate' na kwa hivyo wanalindwa dhidi ya vitu vya mazingira, kama vile kingamwili.

Jamii hizi za bakteria huanzia kwenye meno, ufizi, au ulimi. Katika sehemu zingine kama mashavu, hakuna wakati wa biofilms hizi kuundwa kwa sababu utengenezwaji upya a seli za 'mucosa' hufanyika haraka sana.

Karibu kila eneo la mdomo lina oksijeni tofauti na hali ya virutubisho tofauti, hali inayofanya jamii ya bakteria kubadilika mara kwa mara.

Jamii hii ya bakteria huwa hailingani hata kama iko kwenye jino moja, lakini moja iko mbele na nyuma ya jino hilo hilo. Tofauti hii ni kubwa kiasi kwamba 'microbiota' ya ulimi wako inaweza kufanana zaidi na mtu usiyemjua kuliko kufanana na meno yako mwenyewe.

Kuna vingi zaidi ya kubusu Ukaribu unaotakiwa wakati wa kubusu unasaidia ama unafanya bakteria waweze kusafiri kutoka mdomo mmoja kwenda mwingine. Wengi wao tunawaweza ama kuwatoa bila ya sie kujua.

Bakteria wengi wanaingia mdomoni kupitia kubusu, tunawameza. Uwezo wa bakteria kuishi mdomoni unategemea na namna wanavyoweza kuendena na mazingira yaliyopo ama la.

Kwa kuongezea, mfumo wa kinga, hausaidii kufanya hilo kuwa rahisi, kwa vile mate hufikiria zaidi kingamwili inayoitwa IgA, inayozalishwa na utandao wa Mucous, ambao hujaribu kuzuia kushikamana na bakteria. Kwa ufupi watu ambao wana mashimo kwenye mifumo yao ya meno kwenye mdomo, wanakuwa na kiwango kidogo cha kingamwili hizi.

Kwa hivi, ukimbusu mtu, unapokea bakteria wengi kutoka kwa mtu unayembusu, wengi wa bakteria hao huenda moja kwa moja kwenye utumbo.

Hata hivyo, baadhi hufanikiwa kunata na kusalia kwenye mdomo. Tafsiri ya haya ni kwamba ni ngumu kwa bakteria kuweka makazi mdomono baada ya busu, lakini lazima uwe mwangalifu kwa sababu vipo vijidudu ambavyo sio vizuri vinaweza kujificha kupitia 'microbiota'.

Hatari ya vijidudu hivyo Biofilm inayozalishwa na jamii za bakteria kwenye meno inajulikana kama jalada la meno kwa lugha isiyo rasmi. Wakati mwingine inakuwa ngumu kuliondoa. Bakteria hutumia sukari kwenye chakula na kuzalisha kiwango kikubwa cha kemikali. Hali hii husababisha 'enamel' ya meno kupoteza madini na kusababisha meno kutoboka.

Bakteria kwenye meno wanatofautiana na bakteria wengine waliopo mdomoni. Kwa hivyo matumizi ya sukari yanahusiana moja kwa moja na meno kutoboka ama kuwa na mashimo. Suala hili sio jipya. Kwa mujibu wa rekodi zilizopo, kumekuwa na ongezeko kubwa la meno kuoza, baada ya kodi kwenye sukari kuondolewa nchini England, na jambo hili limekuwa la kawaida. Moja ya bakteria waliobainisha kuleta shida zaidi wanaitwa 'Streptococcus mutans' na aina nyingine ya Lactobacillus.

Je tunaweza kuwaondoa bakteria hawa katika jamii ? Ikiwa kava ama utandu mgumu hautaondolewa kwenye meno, utasababisha kama uvimbe kwenye ufizi ambao huwezwa kurekebishika ikawa ngumu, huharibu tishu maalumu zinazoungana na meno na kusababisha ugonjwa unaoitwa 'periodontitis.

Kwa upande mwingine, hatupaswi kusahau bakteria kadhaa wa jamii hii ya 'microbiota' kwenye mdomo ambao wanahusishwa na halitosis (harufu mbaya inayotokana na mkusanyiko wa bakteria).

Kupiga mswaki meno yako kunasaidia kuzuia kutengenezwa kwa utandu wa meno. Bakteria hawa mara nyingi huishi katika ulimi na huzalisha vitu vinavyochagiza uchomaji wa protini. Kwa hivyo, usafi ni jambo muhimu kupunguza magonjwa yanayoathiri kinywa.

Kwa kupiga mswaki kila baada ya chakula, inasaidia kuondoa 'biofilm' kutoka kwenye 'dental plaque' na bakteria.

Kingine cha kuongezea, unavyopiga mswaki kusafisha meno yako, kunawavutia bakteria wanaohitaji hewa ya Oksijeni ili kuweza kukua, ambalo ni jambo zuri. Unapaswa kupiga mswaki na kusafisha na ulimi wako kwa sababu vitu vinavyosababisha fizi kutoka damu hujificha humo.

Kufurahia maisha ... na kusambaziana 'microbiota' Kwa ujumla, wapenzi walio katika uhusiano imara wanajikuta wanakuwa na aina moja ama inayofanana ya jamii ya bakteria.

Kadri wanavyobusiana ndivyo wanavyopeana bakteria hao na kuwa na bakteria wengi baina yao wanaofanana. Inaweza kuonakana jambo hili kama la kuvutia kwa wapenzi, lakini lina athari yake. Kadri muda unavyokwenda, watu wenye magonjwa ya kinywa wanaweza kuwaambukiza wenza wao.

Watu wenye uhusiano imara na wa muda mrefu hujikuta wanakuwa ana aina moja ya bakteria waliopo mdomoni.

Kwa sasa, utafiti unaendelea kwa ajili ya kuzalisha bidhaa itakayowekwa kwenye kinywa kusaidia kuzuia meno kuoza.

Utafiti wa awali uliofanyika Valencia, umeonyesha kuwa na matokeo mazuri.

Busu linasaidia kuzalisha kichocheo cha mapenzi, kinachoibua hisia na kusaidia kuwaweka pamoja wapenzi kimapenzi. Ukizingatia yote tuliyoyaona kwenye makala haya, unashauriwa kuchagua kwa umakini ni nani unaweza kujenga mahusiano nae na kubadilishana bakteria 'microbes'.

Columnist: BBC