Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Uingereza kwenda Uturuki, kujadili athari za kubadili maumbile

Upasuajiiii (600 X 398) Uingereza kwenda Uturuki, kujadili athari za kubadili maumbile

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia vifo kadhaa vinavyodaiwa kutokana na utalii wa matibabu ya urembo, Serikali ya Uingereza imesema itakutana na maofisa nchini Uturuki kujadili kanuni kuhusu jambo hilo.

Shirika la Habari la Uingereza (BBC) limeripoti kuwa Melissa Kerr 31, alifariki katika hospitali moja binafsi iliyopo katika Jiji la Istanbul, nchini Uturuki mwaka 2019, akiwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili kuongeza makalio (Brazilian butt lift - BBL).

Kutokana na kifo hicho, imeelezwa kuwa mchunguzi wa mwili wa marehemu Melissa, aliibua wasiwasi yeye na wengine kwa sababu hawakuwa wamepewa taarifa za kutosha kabla ya kusafiri nje ya nchi.

Waziri wa Afya wa Uingerereza, Maria Caulfield alisema serikali ilichukulia suala hilo kwa uzito.

Kutokana na majibu kuhusu ripoti ya kuzuia vifo vya siku zijazo iliyoandikwa na mchunguzi mkuu wa miili Norfolk, Jacqueline Lake, Waziri huyo wa afya nchini humo amesema maofisa kutoka idara ya afya na huduma ya jamii watatembelea Uturuki hivi karibuni kukutana na wenzao ili kujadili kwa kina suala hilo.

Ripoti ya Jackqueline imethibitisha kuwa Melissa hakupewa taarifa za kutosha ambazo zingemwezesha kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuamua kufanya BBL. "Hatari kwa raia wanaoendelea kusafiri nje ya nchi kwa taratibu hizo inaendelea... na nina imani kwamba vifo vijavyo vinaweza kuzuilika kwa njia ya utoaji taarifa bora.

Akiwa mama wa watoto watatu, Melissa alifariki Agosti 2020 baada ya kuchomwa ‘liposuction’ nchini Uturuki, ambapo hapo awali, BBC iliripoti jinsi wagonjwa saba wa Uingereza walivyofariki baada ya upasuaji wa kupunguza uzito.

Inaelezwa kuwa mara baada ya kifo cha Melissa, uchunguzi uliofanyika na majibu yake kutolewa mwezi mmoja baadaye, yaliainisha kuwa Melissa alisumbuliwa na donge la damu ambalo lilisafiri hadi kwenye mapafu yake wakati wa upasuaji huo wa kuinua makalio.

Inaelezwa kuwa wachunguzi waliambiwa shughuli za BBL zilikuwa ni za hatari sana, zaidi ya taratibu zote za upasuaji wa urembo. Kwa mantiki hiyo, Uingereza imekubali kusitishwa kwa operesheni kama hizo kutokana na hatari zilizopo.

Waziri Caulfield, alitoa pole kwa familia ya Melissa, huku akisema: "Ni muhimu tujifunze kutokana na kile kilichompata ili kuzuia vifo vya siku zijazo.

Amesema serikali inafahamu ukaguzi uliofanywa na baadhi ya nchi zinazotoa utalii wa matibabu...huenda usilingane na viwango vya udhibiti wa Uingereza, lakini uwazi kwa maana ya kumuelewesha kwa kina anayekwenda kufanyiwa suala hilo ni muhimu ili kupunguza hatari zinazoweza kutokea kwa wagonjwa.

"Ni muhimu sana wale wanaofikiria kufanya utaratibu wa kuinua makalio (BBL) wafahamishwe kikamilifu kuhusu hatari zake, na wawe na wakati wa kutafakari uamuzi wao kabla ya upasuaji.

"Hatari ya kifo kwa upasuaji wa BBL ni angalau mara 10 kuliko taratibu nyingine nyingi za urembo,”amesema.

Serikali ilikuwa inafikiria jinsi ya kuwasilisha kwa ufanisi habari kuhusu hatari za kwenda nje ya nchi kufanya BBL.

Waziri huyo amesema: “Wakati serikali ya Uingereza inachunguza, duniani kote matokeo ya utalii wa kimataifa wa afya...tunaitazama sana Uturuki kutokana na idadi ya raia wa Uingereza wanaosafiri kwenda nchini humo kwa matibabu hayo.

Columnist: www.tanzaniaweb.live