Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ubovu wa viwanja unavyopunguza mabao

Uwanja Wa Mkapa DSM Uwanja wa Benjamin Mkapa

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kama hakuna uwanja, hakuna soka. Nadhani tunakubaliana katika hili. Ni kwa kutambua hilo ndiyo maana wenye mpira wao wakauweka kuwa sheria namba moja katika zile sheria 17 za mchezo huo unaopendwa zaidi duniani.

Lakini unajua kwamba viwanja vinavyotumika kwa mchezo wa soka havilingani urefu na upana? Kwa mujibu wa sheria hiyo, urefu unaweza kuwa kati ya mita 100 hadi 120 na upana mita 50 hadi 90. Sasa tuendelee.

Kwa kutambua umuhimu wake, Mwanaspoti linakudadavulia namna viwanja vilivyotumika katika Ligi Kuu Bara msimu huu 2021/22 vilivyozalisha idadi ya mabao, changamoto zake ambazo baadhi ya wataalamu wameelezea.

UWANJA WA MKAPA – DAR ES SALAAM (63)

Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 katika michezo iliyopigwa hapo jumla ya mabao 63 yalifungwa.

Simba na Yanga ndizo zinazoutumia kama uwanja wa nyumbani, uko chini ya Serikali. Hii ni michezo ya ligi iliyopigwa kwenye uwanja huo na idadi hiyo ya mabao kupatikana.

Michezo yenyewe ni Yanga 1-0 Geita Gold, Simba 1-0 Polisi Tanzania, Yanga 2-0 Azam, Yanga 3-1 Ruvu Shooting, Simba 1-0 Namungo, Simba 2-1 Geita Gold, Yanga 2-1 Biashara United, Yanga 4-0 Dodoma, Simba 2-1 Azam na Simba1-0 Tanzania Prisons.

Michezo mingine ni Simba 1-0 Mbeya Kwanza, Yanga 3-0 Kagera Sugar, Simba 3-0 Biashara United, Simba 2-0 Dodoma, Yanga 2-0 KMC, Yanga 2-1 Namungo, Simba 4-1 Ruvu Shooting, Simba 2-0 Kagera Sugar na Yanga 4-0 Mbeya Kwanza, Simba 3-1 KMC, Yanga 3-0 Coastal, Simba 3-0 Mbeya City, Yanga 2-0 Polisi, Simba 2 vs 0 Mtibwa, Yanga 1-0 Mtibwa.

AZAM COMPLEX – DAR ES SALAAM (56)

Uwanja huu unaomilikiwa na matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC una uwezo wa kuingiza mashabiki 10,000. Mabao yaliyofungwa ni 56 pekee kwa timu tofauti kuutumia kama uwanja wao wa nyumbani.

Michezo iliyozalisha idadi hiyo ya mabao ni Azam 1-0 Namungo, Azam 1-0 Geita Gold, Azam 1-0 Mtibwa Sugar, Azam 2-2 Mbeya City, Azam 4-1 Ruvu Shooting, Azam 2-0 Dodoma, Azam 0-1 Polisi Tanzania, Azam 1-2 Yanga, Azam 2-1 KMC, Azam 1-1 Simba, Azam 2-0 Mbeya Kwanza, KMC 1-1 Biashara United, Ruvu Shooting 1-1 Mbeya Kwanza, KMC 2-0 Dodoma Jiji, KMC 3-0 Polisi Tanzania, KMC 2-0 Geita, KMC 1-1 Ruvu Shooting, KMC 2-3 Coastal, KMC 4-1 Mbeya Kwanza, Azam 2-0 Mbeya Kwanza, Azam 1-0 Tanzania Prisons na Azam 4-1 Biashara.

SOKOINE – MBEYA (55)

Uwanja huu unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi CCM unaingiza mashabiki 20,000. Msimu huu umetumiwa na timu tatu kama uwanja wa nyumbani na umeruhusu mabao 55.

Michezo husika ni Mbeya City 1-0 Tanzania Prisons, Mbeya City 2-2 Mbeya Kwanza, Mbeya Kwanza 1-1 Biashara United, Mbeya Kwanza 2-2 Polisi Tanzania, Mbeya City 3-1 Mtibwa Sugar, Mbeya City 2-2 KMC

Mbeya Kwanza 0-2 Yanga na Mbeya City 2-0 Dodoma, Mbeya Kwanza 0-1 Namungo, Mbeya City 1-0 Simba, Mbeya Kwanza 0-1 Azam, Mbeya City 1-0 Ruvu Shooting, Mbeya Kwanza 1-1 KMC, Mbeya Kwanza 1-2 Mtibwa Sugar.

Mechi nyingine ni Tanzania Prisons 0-1 Ruvu Shooting, Tanzania Prisons 1-1 Mbeya City, Mbeya City 0-1 Kagera Sugar, Mbeya City 0-1 Geita Gold, Mbeya City 1-0 Biashara United, Tanzania Prisons 1-0 Polisi Tanzania, Mbeya City 2-1 Azam, Tanzania Prisons 1-0 Coastal Union,Tanzania Prisons 3-2 Dodoma, Mbeya City 0-1 Coastal Union, Tanzania Prisons 1-1 Geita Gold pamoja na Tanzania Prisons 0-1 Kagera Sugar, Mbeya City 1-1 Yanga, Tanzania Prisons 1-0 Simba.

ILULU - LINDI (43)

Uwanja wa nyumbani wa Namungo FC, unaomilikiwa na Serikali umeruhusu mabao 43 kufungwa tangu ligi hiyo inaanza hadi kumalizika.

Namungo 2-0 Geita Gold, Namungo 1-1 Kagera Sugar, Namungo 1-1 KMC, Namungo 1-1 Yanga, Namungo 1-2 Dodoma, Namungo 1-1 Biashara United, Namungo 3-1 Mtibwa Sugar.

Namungo 2-0 Mbeya City, Namungo 1-2 Azam, Namungo 3-1 Ruvu Shooting, Namungo 2-2 Simba na Namungo 3-3 Tanzania Prisons , Namungo 3-0 Mbeya Kwanza, Namungo 1-2 Polisi Tanzania, Namungo 0-1 Coastal.

MKWAKWANI - TANGA (32)

Uwanja wa nyumbani wa wagosi wa kaya Coastal Union wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 pekee, ni mabao 32 pekee.

Hii ndiyo michezo iliyozaa mabao hayo Coastal Union 1-1 Azam, Coastal Union 2-1 Mbeya Kwanza, Coastal Union 3-2 Mbeya City, Coastal Union 0-1 Mtibwa Sugar, Coastal Union 0-2 Yanga, Coastal Union 1-3 Namungo, Coastal Union 1-3 Ruvu Shooting, Coastal Union 1-2 Simba.

Coastal Union 1-0 Polisi Tanzania, Coastal Union 1-0 Biashara United na Coastal Union 2-1 Dodoma, Coastal Union 0-1 Kagera na Coatal Union 1-1 Geita Gold.

MABATINI - MLANDIZI (26)

Uwanja wa maafande wa Ruvu Shooting hauna hata majukwaa hivyo ni ngumu kuweza kufahamu idadi sawa ya mashabiki wanaoweza kuingia, mabao 26 yamefungwa.

Msimu huu umetumiwa na Mtibwa Sugar pamoja na Ruvu Shooting kama uwanja wao wa nyumbani.

Hizi ndizo mechi zilizochezwa Mtibwa Sugar 0-1 Mbeya Kwanza, Ruvu Shooting 1-0 Coastal Union, Ruvu Shooting 0-1 Polisi Tanzania, Ruvu Shooting 2-1 Kagera Sugar.

Ruvu Shooting 1-2 Namungo, Mtibwa Sugar 2-0 Biashara, United na Mtibwa Sugar 1-1 Polisi Tanzania.

Michezo mingine ni Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting 1-1 Dodoma, Ruvu Shooting 2-1 Geita Gold, Ruvu Shooting 1-1 Azam na Ruvu Shooting 1-1 KMC, Ruvu Shooting 0-1 Mbeya City na Ruvu Shooting 1-0 Tanzania Prisons.

NYANKUMBU - GEITA (29)

Geita Gold moja ya timu zilizopanda daraja msimu huu, imeweza kuwa na uwanja wake wa nyumbani ambao ni mali yao wenyewe, mabao 29 tu yamefungwa.

Geita Gold 1-1 Mtibwa Sugar, Geita Gold 1-1 Mbeya City, Geita Gold 2-1 Ruvu Shooting, Geita Gold 1-0 Tanzania Prisons, Geita Gold 1-1 Mbeya Kwanza, Geita Gold 3-1 Polisi Tanzania, Geita Gold 2-0 Coastal Union, Geita Gold 1-1 Namungo, Geita Gold 2-2 Azam Geita Gold 2-0 KMC na Geita Gold 1-0 Kagera Sugar, Geita 2-0 Dodoma na Geita 2-0 Biashara.

JAMHURI - DODOMA (28)

Mabao 28 pekee yamefungwa katika uwanja huu ulioko makao makuu ya nchi, ukitumiwa na Dodoma Jiji kama uwanja wao wa nyumbani, una uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000.

Michezo iliyozalisha mabao hayo, Dodoma 1-0 Ruvu Shooting, Dodoma 0-1 Simba, Dodoma 2-1 Tanzania Prisons, Dodoma 1-1 Biashara United, Dodoma 1-1 Polisi Tanzania, Dodoma 1-1 Geita Gold, Dodoma 1-2 Kagera Sugar, Dodoma 2-0 Mbeya Kwanza, Dodoma 1-2 Mtibwa Sugar, Dodoma 2-1 Mbeya City, Dodoma 1-0 Namungo na Dodoma 0-2 Yanga, Dodoma Jiji 0-2 Azam na Dodoma Jiji 1-0 KMC.

UHURU - DAR ES SALAAM (17)

Uwanja unaomilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania msimu huu umetumiwa na timu ya KMC una uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000, mabao 17 yamefungwa.

Mechi zilizochezwa ni KMC 0-1 Kagera Sugar, Mtibwa 0-1 Dodoma Jiji, KMC 2-1 Azam, KMC 2-0 Geita Gold, KMC 3-2 Mtibwa Sugar KMC 3-0 Mbeya City, KMC 1-1 Tanzania Prisons.

MANUNGU - MOROGORO (20)

Zaidi ya miaka 20 uwanja huu ulikosa sifa za kutumika katika michezo iliyozihusisha timu kongwe Simba na Yanga.

Sifa ambayo uwanja huo ulikosa ni kukosa majukwaa ambayo yangeweza kutoa nafasi ya mashabiki wengi kuingia hasa Mtibwa inapocheza na Simba au Yanga.

Baada ya kuufanyia kazi upungufu huo msimu huu ulipata baraka zote. Mchezo wao dhidi ya Simba waliyotoka nayo suluhu (0-0) ulipigwa kwenye uwanja huo uliozalisha mabao 20.

Uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 5,000 tu unamilikiwa na Mtibwa Sugar.

Mtibwa Sugar 0-2 Yanga, Mtibwa Sugar 2-0 Geita Gold, Mtibwa Sugar 1-1 Kagera Sugar, Mtibwa Sugar 1-0 Mbeya City na Mtibwa Sugar 1-2 Azam, Mtibwa 3-1 Ruvu Shooting, Mtibwa 2-4 Namungo.

NELSON MANDELA - RUKWA (19)

Uwanja huu umeruhusu mabao 19 katika michezo sita iliyopigwa, unamilikiwa na CCM na una uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000.

Msimu huu Tanzania Prisons ndio ilikuwa ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani. Hii ni michezo iliyozalisha mabao hayo: Tanzania Prisons 0-3 Biashara United, Tanzania Prisons 2-1 Mbeya Kwanza, Tanzania Prisons 3-1 Namungo, Tanzania Prisons 1-2 Yanga, Tanzania Prisons 0-2 KMC na Tanzania Prisons 0-4 Azam.

KAITABA - KAGERA (17)

Wenyeji wa uwanja huu ni Kagera Sugar. Zamani ulikuwa ukimilikiwa na kiwanda cha miwa na sasa uko chini ya halmashauri. Jumla ya mabao 17 yamefungwa.

Una uwezo wa kuingiza mashabiki 5,000 tu. Michezo hii ndio iliyozalisha mabao hayo:

Kagera Sugar 0-1 Yanga, Kagera Sugar 1-0 Mtibwa Sugar, Kagera Sugar 1-2 Geita Gold, Kagera Sugar 1-0 Simba, Kagera Sugar 0-2 Mbeya Kwanza, Kagera Sugar 0-1 Tanzania Prisons, Kagera Sugar 2-1 Coastal Union, Kagera Sugar 1-1 Namungo na Kagera Sugar 1-0 Azam, Kagera 1-1 Dodoma Jiji.

KARUME - MARA (15)

Uwanja huu umeruhusu mabao 15 katika michezo ambayo Biashara United imeutumia uwanja huo wakiwa nyumbani kabla ya kuhamia viwanja vingine.

Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000, mechi zilizozalisha mbao hayo ni Biashara United 0-1 Ruvu Shooting, Biashara United 1-1 Polisi Tanzania, Biashara United 0-1 Coastal Union, Biashara United 3-3 Kagera Sugar, Biashara United 1-0 Mbeya Kwanza, Biashara 1-0 KMC na Biashara United 1-2 Namungo.

CCM KIRUMBA - MWANZA (14)

Uwanja huu unaomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 umezalisha mabao 14.

Michezo iliyozalisha mabao hayo ni Ruvu Shooting 1-3 Simba, Geita Gold 0-1 Yanga, Geita Gold 1-1 Simba, Biashara United 1-1 Yanga, Biashara United 2-0 Azam na Biashara 2-1 Prisons.

USHIRIKA - MOSHI (14)

Uwanja huu mali ya chuo cha ushirika una uwezo wa kuingiza mashabiki 10,000 umewalisha mabao 14.

Polisi Tanzania 2-1Azam, Polisi Tanzania 0-1 Coastal Union, Polisi Tanzania 1-0 Tanzania Prisons, Polisi Tanzania 1-1 Ruvu Shooting, Polisi Tanzania 1-1 Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania 2-0 Biashara United pamoja na Polisi Tanzania 2-0 Mtibwa Sugar, Polisi 0-1 Geita.

NYAMAGANA - MWANZA (7)

Katika mechi tatu zilizopigwa kwenye uwanja huo ambao Biashara United iliutumia kama uwanja wa nyumbani ni mabao saba tu yaliyopatikana.

Biashara United 1-1 Mtibwa Sugar, Biashara United 1-3 Dodoma, Biashara 1-0 Mbeya Kwanza.

MAJIMAJI - RUVUMA (8)

Uwanja huu pia unamilikiwa na CCM, msimu huu umetumiwa na timu ya Mbeya Kwanza kama uwanja wa nyumbani katika michezo kadhaa ni mabao manane tu katika michezo mitano yaliyofungwa.

Una uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000 na michezo iliyozalisha idadi hiyo ya mabao ni Mbeya Kwanza 2-0 Coastal Union, Mbeya Kwanza 1-0 Tanzania Prisons, Mbeya Kwanza 2-0 Kagera Sugar, Mbeya Kwanza 0-1 Geita Gold na KMC 0-2 Yanga.

ALLY HASSAN MWINYI - TABORA (5)

Msimu huu timu ya KMC meutumia katika michezo yake ya nyumbani mabao matano yakifungwa katika uwanja huo.

Ulikuwa mchezo kati ya KMC 1-4 Simba ndio uliopelekea idadi hiyo ya mabao kwenye mechi za Ligi Kuu.

BLACK RHINO - KARATU (2)

Mabao mawili pekee yamefungwa katika uwanja huu ambao Polisi Tanzania ilianza kufungua nao msimu kama uwanja wa nyumbani na baadaye kurejea Ushirika. Polisi Tanzania 2-0 KMC

SHEIKH AMRI ABEID - ARUSHA (1)

Uwanja huu unamilikiwa na CCM umetumiwa na Polisi Tanzania kama uwanja wa nyumbani katika mchezo mmoja na bao moja pekee ndilo limefungwa. Polisi Tanzania 0-1 Yanga.

SIFA ZA VIWANJA VYA LIGI KUU

Ili uwanja utumike katika michezo ya Ligi Kuu unahitaji kuwa na vitu hivi, sehemu nzuri ya kuchezea (pitch), vyumba vya kubadilishia nguo, chumba cha huduma ya kwanza, chumba cha mikutano ya waandishi wa habari, vyoo vya mashabiki.

Vigezo vingine uwanja unatakiwa kuwa na majukwaa ya kukaa watazamaji, sehemu ya kuegesha magari, chumba cha dawa.

Meneja anayesimamia leseni za klabu, Jonas Kiwia anasema sababu za kuvifungia viwanja hivyo baada ya ukaguzi: “Changamoto kubwa ya viwanja vyetu mkikagua leo uwanja uko poa kesho ukitumika kwa kazi nyingine mfano gwaride, ama majukumu yasiyo ya kimpira unaharibika na ndio unasababisha kufungiwa.”

KAULI ZA WACHEZAJI

Mfungaji Bora wa msimu huu, George Mpole na winga Juma Mahadhi wote Geita Gold wanasema, changamoto za viwanja zinafanya mchezaji acheze kwa tahadhari kubwa ili aweze kuepuka majeraha yanayoweza kurudisha nyuma kiwango chake.

“Mimi nilipambana iwe kiwanja kibovu au kizuri kuhakikisha lengo langu linatimia, kwa uwezo wa Mungu nilifanikiwa lakini ubovu wa viwanja unamfanya mchezaji ashindwe kuonyesha uwezo wake, na hii ndiyo hali halisi ya nchi yetu tunapambana hivyo hivyo,” anasema Mpole.

“Viwanja kama Karume, Mabatini, Jamhuri Dodoma, Sokoine pamoja na CCM Kirumba ni vibaya. Benjamin Mkapa, Uhuru, Chamazi na Kaitaba vinakufanya mchezaji uweze kufunga na kuonyesha uwezo wako vizuri,” anasema Mahadhi.

Mbaraka Yusuph mshambuliaji wa Kagera Sugar anasema changamoto ya viwanja ni kubwa katika ligi ya Tanzania, hata wao wanalazimika kukabiliana nayo na kucheza.

Beki wa Geita Gold, Adeyum Saleh anasema kuna tofauti kubwa Uwanja wa Mkapa na viwanja vingine vinavyotumika katika Ligi Kuu.

Columnist: Mwanaspoti