Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ubia wa REA inaposhikamana na Wakala Misitu kuwasha umeme

REA Ubia wa REA inaposhikamana na Wakala Misitu kuwasha umeme

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umeme ‘bwelele’ vijijini, nguzo za nyumbani Wawekezaji nguzo kibao ‘mteja wa uhakika’

NI miaka mitano sasa, kuna hatua kubwa imepigwa katika usambazaji umeme nchini, hasa katika dhana kuu ya kuufikisha katika vijiji vingi kitaifa.

Mdau mkuu hapo ni Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kazi hiyo ikifanyika kwa taratibu na gharama nafuu zaidi chini ya malezi makuu ya kisera kutoka serikalini, mlezi na msimamizi mkuu Wizara ya Nishati.

Ni mradi unaofanyika kwa awamu kuzunguka maeneo mbalimbali ya vijijini, mtazamo mkuu ni kumaliza kila kona ya vijijini kitaifa.

Ni kazi ya kiufundi inayofanywa na REA, ikihusisha matumizi ya rasilimali nyingi kama fedha, nguvu kazi na vifaa vya umeme kama nyaya za na nguzo za kusafirisha umeme.

KAZI YA TFS

Ili kufanikisha, kunaibuka hitaji la vifaa hivyo vipatikane kwa wakati na gharama nafuu. Hapo ndipo panatokea hitaji la sekta misitu, mhusika na mnufaika mkuu katika utoaji mchango chanya katika jitihada za serikali na usambazaji umeme.

Sekta misitu ina manufaa katika maeneo makuu mawili. Kwanza, upatikanaji malighafi ya nguzo zenye ubora na kubwa tofauti; pili kuruhusu umeme kupita katika maeneo ya misitu bila ya fidia.

Misitu ya serikali inayozalisha nguzo imenufaika sana na biashara ya miti ya kutengenezea nguzo, hali kadhalika mashamba ya wananchi na asasi nyingine binafsi.

Mashamba ya miti ya serikali yanayosimamiwa na kuendelezwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), yamekuwa mstari wa mbele katika ufanisi wa kutoa miti bora ya kutengenezea nguzo za umeme.

Baada ya kuliona hilo, TFS nayo imekuwa ikijitahidi kupanda miti mipya kila baada ya mavuno, kuhakikisha nguzo zinazohitajiwa na REA zinapatikana wakati wote kwa namna endelevu.

Kamishna wa TFS, Dos Santos Silayo, anasema wanahudumia wateja 186, wakiwamo Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), inayovunwa kutoka mashamba yake nchini.

Anasema wateja hao huvuna wastani wa nguzo zenye ukubwa wa mita za ujazo 150,000 kwa mwaka, ikiwa biashara iliyoibua fursa kubwa katika uwekezaji wa misitu nchini, ikihususha wadau mbalimbali.

Silayo anatumia fursa hiyo kusifu uamuzi wa serikali kuuwekeza kwenye teknolojia ya kutibu nguzo na anarejea takwimu za ndani ya kuwapo uwezo wa viwanda kuruhusu umeme kupita katika misitu bila ya fidia.

Hadi sasa inaleezwa ni hatua kubwa inayopigwa ikizingatiwa nguzo hizo zinazozalishwa nchini, awali ziliagizwa kutoa nje ya nchi.

Miti hutumia hewa chafu ya ukaa kutengeneza chakula chake na kisha miti hiyo inapotumika kama malighafi huhifadhi kaboni kwa muda mrefu bila kuiachia angani.

TFS, inawapongeza waliowekeza katika malighafi nguzo, akizitaja kampuni za misitu zilizowekeza katika uzalishaji wake nchini, hali inayoiwezesha nchi kuwapiku washindani wakongwe, viwanda vya Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako bidhaa hizo zilozgizwa awali.

Uamuzi wa kutumia nguzo za ndani ulitolewa na serikali na kuachana na dai la kwamba ‘nguzo za nchini hazina ubora’ na matinda yake ya sasa, ni kwamba biashara hiyo imeongezeka maradufu na nyenzo ya kukabili tabia nchi.

Silayo anakumbusha wajibu wa umma, kila mmoja anapaswa kuzingatia wajibu wa kutunza misitu iliyopo, ili isaidie kutoa nguzo za umeme zinzotumiwa kwa ajili ya kuwawekea watu umeme katika maeneo ya mijini na vijijini.

Kamishna Silayo anasistiza wito wa TFS, kwamba kila mwananchi ahakikishe anakuwa mlinzi wa mwenzake, katika kuhakikisha ibaki salama.

WADAU MISITU

Mmoja wa wananchi wanaoishi jirani na misitu, Jerome Massawe, anaunga mkono hoja hiyo, akihimiza kwamba misitu inapaswa kuheshimiwa na kutunzwa, kwa sababu ni mzizi wa faida kubwa kwa wananchi na taifa kwa jumla.

“Bila misitu, hatuwezi kupata miti ambayo itatengenezwa nguzo za umeme, hatuwezi kupata mbao ambazo hutumika kutengeneza fenicha mbalimbali ambazo huitajika katika matumizi ya binadamu,” anasema.

Asia Juma, mdau mwingime wa rasilimali misitu anasema wananchi wana kila sababu ya kutunza misitu inayowazunguka, kwa sababu ina faida kubwa kuanzia ndani ya jamii yao, hata taifa kwa jumla.

Mama huyo anaorodhesha faida hizo mtambuka, zinazojumuisha uchumi na mazingira, anazitaja kuwa inaleta mvua, hali ya hewa nzuri na matumizi na malighafi kwa mengi ya miradi ya kiuchumi na kibiashara.

Kutokana na mustakabali huo, Asia anahimiza jamii kuzingatia utunzaji na kuheshimu misitu kila wakati na njia mojawapo anayoshauri ni kwamba kila anyemuona mkata misitu ovyo jirani, anapaswa kuchukua hatua ya kumripoti haraka katika mamlaka husika za kiserikali zinazosimamia hifadhi zake, ili hatua sahihi ichukuliwe.

Columnist: www.tanzaniaweb.live