Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Nenda Cedrick Kaze, huo ndiyo mpira wetu Bongo

Kazee Kutokea Data UCHAMBUZI: Nenda Cedrick Kaze, huo ndiyo mpira wetu Bongo

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Mwanahiba RichardMore by this Author FEBRUARI 3, mwaka huu ni siku ambayo timu ya Mwanaspoti tulialikwa kwenye kambi ya Yanga huko Kigamboni, mwaliko huo ulikuwa ni wa kocha Cedrick Kaze baada ya kumuomba kufanya naye mahojiano. Nikiwa na jopo la waandishi wenzangu watatu hivyo kuwa idadi ya watu wanne, tulifika kwa muda ambao alitupangia kulingana na ratiba yake ingawa tuliwahi kidogo ili tusije tukachelewa kutokana na miundombinu yetu ya usafiri hapa Dar es Salaam.

Hatukukurupuka kwenda, kwani kabla ya yote tulifuata taratibu zote za kuhojiana na kocha huyo kuanzia kwa viongozi wake ambao walitoa baraka za sisi kuzungumza na Kaze.

Tulipokewa vizuri na wale tuliowakuta kabla ya kuonana na kocha ambapo baadaye aliwaagiza tupelekwe kwake na ikawa hivyo. Siku hiyo alikuwa na jukumu la mechi ya kirafiki hivyo alitueleza mahojiano yanapaswa yatumie dakika 30 ili aendelee na ratiba yake. Hatukuwa na pingamizi kwani hata sisi tulijiandaa vyema kwa maswali ambayo yote aliyajibu pasipo kupepesa macho.

Moja ya swali tulilomuuliza ni kwamba endapo timu itafanya vibaya kwa maana ya kwamba ikitokea ikiwa na matokeo mabaya ambayo yakawakasirisha mabosi na mashabiki wa Yanga atachukuwa uamuzi gani.

Kaze alijibu mashabiki na viongozi wanapaswa kutambua kwamba mpira una matokeo matatu, kushinda, sare na kufungwa, wakati huo Yanga ilikuwa haijapoteza mechi hata moja, bali kulikuwa na sare na maneno ya chinichini yalizungumzwa kwamba hawafurahishwi na kiwango cha timu. Aliulizwa tena, makocha wengi hufukuzwa kwenye timu zinapofanya vibaya au kuona kiwango cha timu hakiridhishi hata kama timu inapata matokeo itakuwaje, akajibu hali hiyo ipo duniani kote hivyo haitakuwa ajabu.

Tuliuliza tena, kuna baadhi ya timu viongozi hupenda kuingilia majukumu ya makocha, na makocha wakigoma kuingiliwa majukumu yao, basi hutimuliwa kwako ikoje, akajibu akiwa kama kocha ana misingi na misimamo yake, hivyo hatakubali kuingiliwa majukumu na atasimamia msimamo wake wa kile anachokiamini katika majukumu yake. Sasa basi, majibu ya Kaze binafsi nilikubaliana nayo kwasababu hiyo ndiyo kaze yake na ameisomea na ndiyo maana alipata ajira ndani ya Yanga haijalishi alikuwa anapata matokeo gani na timu ilikuwa inachezaje. Bali hicho ndicho alikiamini hata yeye ndiyo maana alijibu kwa kujiamini.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz