Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Namungo inastahili pongezi kwa hatua iliyofikia Afrika

Namungo Pic 1 Data UCHAMBUZI: Namungo inastahili pongezi kwa hatua iliyofikia Afrika

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

HUU ni msimu wa pili kwa Namungo FC kushiriki Ligi Kuu Bara, imekuwa ikifanya vizuri kwenye ligi hasa msimu wa kwanza ingawa msimu wa pili ilianza kwa kusuasua kidogo.

Msimu uliopita Namungo ilipata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kufika hatua ya fainali ambapo walicheza na Simba iliyotwaa ubingwa huo wa Kombe la Shirikisho la Azam.

Wakati Simba inatwaa ubingwa huo wa FA, tayari ilikuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo ilikuwa ni lazima Namungo walioshika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo ndiyo washiriki michuano ya Afrika.

Namungo iliingia kwenye michuano hiyo kama utani kutokana na namna kikosi chao kilivyokuwa kinapata matokeo ambayo hayakuwa ya kuridhisha baada ya kufanya usajili usiokuwa wa kutisha kama ilivyokuwa timu zingine zinaposhiriki mashindano makubwa.

Timu hiyo yenye maskani yake Ruangwa ilianza kupambana kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika kama utani hadi ilipofikia hatua ya mwisho ya mchujo ili kuingia makundi.

Haikuwa safari nyepesi kwa Namungo kufikia hatua hiyo, imekutana na changamoto za hapa na pale ikiwemo kushindwa kucheza nchini Angola baada ya kutolewa taarifa na wenyeji wao kwamba wachezaji Fredy Tangalo, Lucas Kikoti, Hamis Mgunya pamoja na mtendaji mkuu Omary Kaaya kukutwa na virusi vya corona, hivyo wakataka timu nzima ikae karantini.

Related Kifungo cha Mwakalebela ni kianzio tosha kwa Dk Abbas MZAMIRU: Tuna Luis, Chama tunakosaje ubingwa?Jambo hilo liligomewa na viongozi wa Namungo ambapo iliwabidi wakae kwenye gari, hali iliyosababisha mchezo huo kufutwa kabla ya maamuzi ya kamati ya Caf kuruhusu mechi zote mbili zichezwe Tanzania.

Namungo imeshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo na imeweza kuonyesha uwezo wa kufika hatua nzuri ya makundi ingawa awali ni timu iliyokuwa inabezwa kutokana na kikosi chao kilivyo na ugumu wa mashindano hayo.

Wakati michuano hiyo inaanza viongozi wa Namungo kupitia kwa Katibu Suleiman, alikaririwa kwamba bajeti yao ilikuwa Sh500 milioni ingawa hawakuwa na uhakika wa kufika hatua ya makundi.

Pamoja na bajeti yao finyu Namungo walipambana kwani katika mechi nne walizocheza awali walifunga mabao 14, huku straika wao Stephen Sey akiwa anaongoza kwa kufunga mabao matano, jambo linaloonyesha ni timu yenye washambuliaji wazuri.

Matokeo yao katika mchezo wa kwanza dhidi ya Al Rabita iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliofungwa na Sey (katika dakika za 20 na 38) na Shiza Kichuya (61) ambapo mchezo wa marudio uliopangwa upigwe Desemba 6, 2020 Al Rabita haikutimiza vigezo hivyo Namungo ikapewa ushindi wa mezani.

Namungo iliendeleza ubabe wake baada ya Desemba 23, 2020 kuichapa Hilal Obayed mabao 2-0 yaliofungwa na Sixtus Sabilo (dakika ya 13) na Sey (dakika ya 31), ambapo Januari 5, 2021 ilitoka sare ya mabao 3-3 wafungaji wakiwa ni Sey (dakika 2), Blaise Bigirimana (38) na Edward Manyama (50).

Wakati mchezo wake wa mwisho imekipiga na 1 de Agosto ikiwa ndio mwenyeji wa mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Chamazi, Namungo ilishinda mabao 6-2 yaliofungwa na Hashim Manyanya (dakika 32), Sabilo (38, 59), Reliants Lusajo (55), Eric Kwizera(66) na Sey dakika (71).

Namungo ilitinga hatua ya makundi ambapo imepoteza mechi zake zote tatu dhidi ya Raja Casablanca bao 1-0, Pyramids bao 2-0 na Nkana bao 1-0.

Hivi sasa Namungo watakwenda kucheza mechi za ugenini ambapo ni ngumu na ngumu kweli hasa kutokana na matokeo yao ya awali ambayo hayawapi mwanga wa kusonga mbele zaidi.

Ni wazi kwamba Namungo safari yao imeishia hapo kwani huko mbele ni kugumu na kuna giza kubwa, hawawezi kupenya tena ila tunapaswa kuwapongeza kwa hatua waliyofikia maana kwa timu changa ni hatua kubwa kufika hatua hiyo.

Namungo ilianza mashindano hayo kila mmoja aliibeza kwamba ingetolewa hatua ya awali tu lakini ni kama iliwashangaza wengi kufika hadi hatua ya makundi, hivyo kwani wamejifunza mengi na watakuwa wamekomaa kiufundi kutokana na kukutana na

timu nyingi kubwa na zenye wachezaji wazoefu.

Hatupaswi kuwabeza Namungo kwa kupoteza mechi zote za mzunguko wa kwanza wa makundi bali tuwapongeze kwa hatua waliyofikia kwani ni hatua kubwa ambayo pengine wakipata tena nafasi watafanya vizuri kwa kuwa watakuwa wamepata uzoefu.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz