Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Magufuli ametangulia,makatazo yake yaishi michezoni

Tff Pic Data UCHAMBUZI: Magufuli ametangulia,makatazo yake yaishi michezoni

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TAIFA la Tanzania bado lipo katika nyakati ngumu za kuondokewa na aliyekuwa Rais wa tano, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo kufuatia kuugua kwa siku chache.

Siku ngumu kwa Watanzania itakuwa ni leo wakati Rais Magufuli atakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ndio mwisho wa safari yake hapa duniani.

Kinachowaliza maelfu ya watu sio kifo cha JPM, bali wanakumbuka mambo ambayo aliyafanya enzi za uhai wake hasa nyakati ambazo alizonyesha mtu ambaye alijua upungufu wa aina gani ambao taifa linaangamia kwa uwepo wake.

Katika kipindi cha miaka sita JPM alifanikiwa kubadilisha mambo mengi na taifa likaishi kwa misimamo yake kwa kila idara kuogopa kivuli chake wakijua anayoyataka yafanyike kwani hakuwa mtu ambaye anasita kuchukua.

Haikuwa ajabu kuona JPM akimchomoa mtu katika nafasi yake kwa makosa ya kikazi au ubabaishaji ambao hakuutaka kuona unachukua nafasi katika utawala wake na hapo inawezekaana kila mmoja anayekumbuka mambo yake anajikuta analia au kuumizwa na kifo chake. JPM hayupo tena na taifa zima kesho litakuwa bize likifuatilia ukamilifu wa safari yake hapa duniani, huku akiwa ametuachia ujumbe mzito wa jinsi gani tunatakiwa kujitathimini katika kuendeleza yale ambayo aliyaona ni mwiba katika kutamani taafa lipate maendeleo.

Huku kwenye michezo nako yapo mambo ambayo aliyafanya enzi za uhai wake ambayo inawezekana uwepo wake ulisaidia baadhi ya mambo kuonekana yanapiga hatua kwa namna moja au nyingine.

Related UCHAMBUZI: Simba hakikisheni kwamba mnalipa deni la MagufuliKwa nafasi fulani kulikuwa na woga katika kuzidisha weledi katika uongozi na maisha ya idara nyingi za michezo yalibadilika, ulafi wa fedha ulipungua kutokana na kuwa hakuweza kusita kutoa kauli kali hata mbele ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akitaka kuona matumizi ya fedha ambazo anazitoa yanakwenda kutumika vizuri.

Kauli ile ilisaidia kuhakikisha viongozi wengi wa michezo wanakuwa na woga katika fedha za umma kwa kuwa aliipa meno Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuweza kuingia kokote na kuyafanyia kazi mambo ambayo wanayaona hayapo sawa.

JPM pia alitamani sana kuona timu zinapata mafanikio katika mashindano yao na sio kuwa wasindikizaji katika kila mechi ambazo wanacheza. Alitaka kuona kila timu inajiandaa kisawasawa kabla ya kwenda mashindanoni.

Nidhamu hiyo ikaleta mafanikio katika utawala wake timu nyingi za taifa zilirudisha ubora kwa kushiriki mashindano makubwa ya Afrika kuanzia Taifa Stars ambayo ilirejea katika ushiriki wa Fainali za Mataifa Afrika (Afcon) kule Misri, lakini pia timu za vijana katika umri mbalimbali nazo zilifuzu fainali kama hizo.

Ngazi ya klabu nako mambo yalikuwa hivyohivyo angalia sasa Simba ikionyesha kiwango bora ambacho wenyewe wamekiri kwamba maneno ya JPM ndio yalikuwa dira kubwa ya kuamua kuweka mkazo wa kuhakikisha wanayapata mafanikio hayo lakini pia klabu zingine kama Mtibwa Sugar na sasa Namungo nazo ziliingia katika historia ya kufuzu mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kuondoka kwa JPM hakupaswi kuishia hapo kwa msisitizo wake wa kutaka kuona umakini kama huo unazidi kuendelea kuchukua nafasi na badala yake tukarudi katika ubabaishaji ambao ulikuwa sehemu kubwa ya maisha yetu huko nyuma.

JPM alituonyesha njia na sasa tunatakiwa kuendelea kuishi humo katika safari yetu na sio tena kuacha ambayo alitufundisha kisha tukaanza kuporomoka kwa kasi. Njia nzuri ya kumuenzi kiongozi huyo ni kuhakikisha kila idara inaendelea kuwa imara na kutafuta mafanikio zaidi.

Nilifurahia kauli ya Rais aliyechukua hatamu kutoka kwa JPM, Mama Samia Suluhu Hassan juzi pale Dodoma akilihakikishia Taifa kwamba wanaodhani nchi haina Rais basi yupo na ni Rais kamili kama aliyemtangulia.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz