Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Kaze sawa, tusisahau Yanga ilianguka maeneo mengi

Pic Kaze Data UCHAMBUZI: Kaze sawa, tusisahau Yanga ilianguka maeneo mengi

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author UPEPO bado haujatulia ndani ya Yanga presha ya maisha yao imekuwa ikibadilika kila baada ya muda kutokana na maisha ambayo wameamua kuishi ndani ya klabu ambayo hivi karibuni imewatimua makocha wake watatu na ofisa usalama.

Uamuzi huo umetokana na kupepesuka kwa kikosi katika mechi saba walizocheza wakishinda mbili, sare nne, na mwisho wakipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu tangu msimu uanze.

Tayari mtu ambaye aliimbwa kama wimbo mbaya kocha Cedric Kaze yuko nje ya ajira kutokana na mwenendo wa kikosi akiwa mhanga wa kwanza, lakini pia akiongozana na wasaidizi wake watatu.

Kumfukuza Kaze inawezekana ukawa uamuzi sahihi kwa kuwa timu iliyumba kimatokeo ndani ya muda mfupi eneo ambalo yeye ndiye bosi mkuu anayetakiwa kuhakikisha matokeo yanapatikana - kwa hiyo huwezi kuwalaumu viongozi wa Yanga kwa hatua hiyo.

Yanga inapaswa itulie kunahitajika kufanyika uamuzi wa zaidi ya kumfukuza Kaze kwani yapo maeneo mengi hayakuwa na afya ya kuweza kuleta utulivu wa kuwa kama klabu kubwa inavyotakiwa kujiendesha katika kazi zake.

Baada ya Kaze, naamini ngazi ya juu ya klabu itaenda mbali zaidi kwa hata kujiangalia yenyewe wako katika utulivu wa namna gani? Je uongozi wao una upungufu kiasi gani na jinsi gani watajinasua endapo watabaini changamoto mbalimbali?

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz