Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

UCHAMBUZI: Gomez anarudia kilichofanya Sven achukiwe

Gomez Pix Data UCHAMBUZI: Gomez anarudia kilichofanya Sven achukiwe

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelMore by this Author HADI anaondoka nchini kuelekea Morocco, kocha Sven Vandenbroeck hakuwa anapendwa na kundi kubwa la mashabiki wa Simba.

Wengi wao walianza kumzungumza vizuri baada ya kuachana na timu hiyo ghafla na kwenda Morocco alikojiunga na FAR Rabat, moja ya timu kubwa nchini humo ambayo ilivutiwa na kile alichokifanya ndani ya Simba.

Kabla ya yeye kuiwahi Simba na kuondoka, kundi kubwa la watu ndani ya Simba lilikuwa linatamani klabu hiyo imtimue na iajiri kocha mwingine licha ya kuwapatia mataji matatu makubwa kwa muda alioinoa ambayo ni Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam lakini kubwa zaidi, ndiye kocha aliyewaongoza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wanatamba nayo hivi sasa.

Hapana shaka sababu kubwa ambayo iliwafanya watu wengi wa Simba kumchukia Sven ilikuwa ni kitendo chake cha kutompa nafasi mara kwa mara mshambuliaji wake, Meddie Kagere ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo zilizopita.

Wengi hawakuwa wakipendezwa na mbinu ya kocha huyo raia wa Ubelgiji, kutumia mfumo wa 4-2-3-1 wa kusimamisha mshambuliaji mmoja mbele kwa sababu ulikuwa hautoi nafasi ya kutosha kwa Kagere kucheza na badala yake akawa anatumika zaidi John Bocco au Chris Mugalu.

Sven alikuwa anaamini Simba ikicheza ikiwa imejaza idadi kubwa ya viungo, inakuwa salama zaidi kwa maana ya ulinzi lakini pia katika kutengeneza nafasi lakini hakuwa anaeleweka na wengi ambao walikuwa wanamuwaza zaidi Kagere.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz