Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tutunze miundombinu, tutumie fursa ya elimu

534b226864d9f8de81dd58cac8e29a98 Tutunze miundombinu, tutumie fursa ya elimu

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TANGU iingie madarakani mwaka 2015, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John magufuli, ilitilia mkazo utumishi uliotukuka na uwajibikaji wa viongozi, watendaji na kila mmoja katika eneo lake ili kumaliza kero za wananchi.

Maeneo ambayo serikali imeyawekea nguvu kati ya mengi, ni pamoja na kuwekeza katika upatikanaji wa huduma za maji safi na salama sambamba na kelimu bila malipo inayotolewa ili hata watoto maskini wapate haki hiyo.

Awali, changamoto kubwa walizokabiliana nazo Watanzania zilikuwa ni pamoja na ukosefu wa uhakika wa upatikanaji wa huduma mbalimbali zikiwamo za maji safi, umeme, afya na baadhi ya familia kushindwa kumudu gharama za elimu hata ya msingi kwa watoto wao.

Uwepo wa ada na michango mbalimbali ya elimu kwa shule za msingi na sekondari ulikuwa kikwazo kwa familia nyingi huku pia, ukichochea utoro na ongezeko la watoto wanaoshindwa kumaliza elimu ya msingi au sekondari.

Kukosekana kwa huduma za maji kulisababisha kuzuka kwa kundi la wauza maji kwa njia ya madumu hasa maeneo ya mjini kiasi kwamba, katika baadhi ya maeneo, dumu moja la maji liliuzwa kati ya Sh 500 hadi Sh 1,000, hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa watu.

Ukosefu huu ulisababisha kuzuka kwa wizi wa maji kupitia uchepushaji kwa watu waliojijengea visima vikubwa nyumbani na kuuza maji rejareja kwa watumiaji wa kawaida.

Hii ni kwa kuwa mara nyingi walitumia muda wa kufuatilia masomo, kwa ajili ya kutafuta maji.

Kimsingi, mateso yalikuwa yanazidi kwa kuwa wokovu ulikuwa unakaribia na sasa umewadia kwa Watanzania.

Kimsingi, Serikali inaendelea kutekeleza sera ya elimu bila malipo na upatikanaji wa huduma nyingine na uboreshaji wa miundombinu ikiwamo ya maji na umeme unazidi kuongezeka na kuimarika.

Hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi, alianika bayana kuthibitisha namna serikali inavyopambana na kutumia trilioni za Shilingi za Tanzania kutekelez miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za jamii zikiwamo za maji na elimu.

Katika taarifa hiyo, Dk Abbasi anasema hadi sasa Serikali imetumia Sh trilioni 1.916 kutekeleza miradi 1,845 tangu mwaka 2015.

Anasema katika kipindi cha Magufuli, Sh trilioni 1.291 zimetumika kugharimia elimu ya msingi bila malipo na kusaidia maelfu ya watoto kwenda shule kupata haki stahiki. Hili linahitaji shukurani na pongezi kwa Rais Magufuli maana ametekeleza.

Ni haki na wajibu wa Watanzania kutunza miundombinu yote ikiwamo ya maji, umeme, elimu na mingine, huku ikitumia utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo kama fursa kwa watoto kupata haki ya elimu ambayo kama si Rais magufuli, huenda wasingeipata.

Columnist: www.habarileo.co.tz