Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tutunze maliasili kwa maslahi ya vizazi vijavyo

Fe5fb77a2c5dba87db3956302dc73f08 Tutunze maliasili kwa maslahi ya vizazi vijavyo

Mon, 18 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TANZANIA imejaliwa na utajiri unatosha kuifanya ipae kimaendeleo na badala ya kunyatanyata. Utajiri huo unajumuisha rasilimali mbalimbali kama vile watu, maliasili na ardhi nzuri na ya kutosha kwa kilimo na shughuli nyingine mbalimbali.

Matumizi na malengo ya utajiri huo kimsingi yanatakiwa yalenge kuwatajirisha Watanzania wa leo na Watanzania wa vizazi vijavyo.

Ili kuweza kuyafikia malengo hayo tunatakiwa kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali hizo.

Matumizi mazuri ni ya rasilimali yanajumuisha utunzaji wa rasilimali hizo ili zidumu kwa muda mrefu na hatimaye, kuwafikia vizazi vijavyo hata vya miaka 100 ijayo.

Ili kuweza kutunza rasilimali za nchi hii, lazima kila mwananchi awe mstari wa mbele kuzitunza na kuhakikisha hazitumiki vibaya, wala kuchukuliwa na wajanja wachache wakiwamo mabeberu wan je wanaotumia baadhi ya Watanzania waliokufa moyo wa uzalendo.

Kuwa mstari wa mbele katika kutunza rasilimali za nchi ni pamoja na kushiriki kivitendo kupiga vita uharibifu wowote wa maliasili au matumizi mabaya ya maliasili za nchi,

Kimsingi bila kushirikiana kila mmoja kwa nafasi hyake, hatuwezi kuyafikia malengo tuliyojiwekea ya kuwatajirisha watoto wetu waliopo sasa na hata wale ambao hawajazaliwa.

Wataznania tuwe watu wanaothamini watoto wa leo na kesho kwa kuwa na hulka ya kutumia kilichopo kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo kwa kuwa tunawathamini watoto wa leo na wa kesho.

Mwalimu Julius Nyerere alithamini watoto wote wa wakati huo mwanzoni mwa kujitawala na aliwathamini watoto ambao walikuwa hawajazaliwa. Ndiyo maana alitunza rasilimali za nchi hii na kuzitumia kwa maslahi ya Watanzania wote.

Watanzania wote tunatakiwa kutunza rasilimali na nchi hii ili ziwafae pia Watanzania watakaokuja hata baada yetu yaani, Watanzania watakaozaliwa miaka 100 ijao kama alivyofanya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Kwa msingi huo, kila mmoja mahali alipo, awe balozi bora wa utunzaji wa rasilimali za taifa yakiwamo madini, wanyamaporina mazao ya maliasili za misitu na bahari.

Kila mmoja afuate sheria za nchi zinazotoa mwongozo kuhusu rasilimali za nchi kama vile ardhi, mbuga za wanyama, milima, mito, maziwa, mabonde na bahari.

Kila mmoja bila hiyana, awe makini na tayari kufichua yeyote anayetaka kujifaidisha na kufaidi kikundi cha watu ama ndani au nje ya nchi kwa gharama ya hasara kwa taifa

Watu wanaofanya shughuli za kilimo katika vyanzo vya maji kama vile chemichemi na mito waelimishwe kuhama na ikibidi, wapewa onyo kali au adhabu ili kuwalazimisha kuacha uharibifu wa mazingira.

Kila mmoja atambue kuwa, vizazi vijavyo havitakuwa katika neema kama watu wataruhusuiwa kulima kando kando ya vyanzo vya maji kama chemichemi.

Wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika mbuga za wanyama kwa kisingizio cha kukosekana malisho katika maeneo yao, watambue kuwa wanalikosea taifa na wanahatarisha hifadhi hizo kwa wanyama kukimbia, kuhama na wemngine kuambukizwa magonjwa kutoka kwa mifugo.

Jamii yaani wananchi, waungane na mamlaka katika maeneo yao na vyombo vya usalama kutekeleza wajibu wao kisheria ili kuhakikisha hakuna mtu anayeharibu rasilimali za nchi.

Columnist: habarileo.co.tz