Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

‘Tutamkumbuka Dk Magufuli kwa morali aliyotupa’

6cce4caedd1bce65ab9014cb96d5f183.jpeg ‘Tutamkumbuka Dk Magufuli kwa morali aliyotupa’

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WADAU mbalimbali mkoani Arusha wamesema kuwa watamuenzi Rais Dk John Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii kwani hiyo ndio ilikuwa kauli mbiu yake kipindi chote cha uongozi wake akiwa Rais.

Walisema Magufuli alikuwa akihimiza Watanzania kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu" na kuhamasisha uchumi wa viwanda ambao uliwapelekea vijana wengi kujiajiri na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Akizungumzia namna ambavyo Rais Magufuli alihakikisha watu wanajituma na kufanya kazi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Okoa New Generation inayojishughulisha na utetezi wa masuala ya vijana ,wanawake na walemavu, Neema Mgendi alisema kuwa Magufuli alitoa morali kubwa sana kwa Watanzania kufanya kazi kwa bidii katika kufikia uchumi wa viwanda.

Neema alisema kuwa, Rais Magufuli aliweka nidhamu kubwa katika Taasisi mbalimbali za umma na serikali na alifanya pawepo kwa nidhamu kubwa na kupunguza uzembe na kufanya kazi kwa mazoea uliokuwa ukifanywa na viongozi katika Taasisi na makampuni mbalimbali .

Alisema kuwa watamkumbuka kwa namna ambavyo aliwezesha wamachinga kupata vitambulisho na kufanya shughuli zao bila usumbufu wowote bila kubughudhiwa na mtu yoyote na hatimaye kuweza kuondoa Kodi zisizo rasmi.

“Kwa kweli Magufuli alifanya watu kuwa na nidhamu ya hali ya juu,ile tumbua tumbua ilisaidia sana kwani watu waliogopa wakawa wanafanya kazi kwa kujituma na kuacha uzembe kwa kweli tutamkumbuka kwa mambo mengi sana na tunaomba viongozi waliopo waendelee kuyaenzi na kuyaendeleza yale yote yaliyofanywa,” alisema.

Meneja wa Sido, mkoa wa Arusha Nina Nchimbi alisema kuwa watamkumbuka Rais Magufuli kwa namna ambavyo alihakikisha uchumi wa viwanda unaendelezwa na hivyo kuwawezesha vijana mbalimbali kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuweza kujiajiri katika sekta ya viwanda.

Columnist: www.habarileo.co.tz