Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tusitafute njia mkato Afrika

Hilal Vs Yanga 1 0.jpeg Tusitafute njia mkato Afrika

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Waswahili wanasema kila nafsi itaonja umauti. Hii haijarishi kama nafsi hii inaenda peponi au jahanamu. Maana yake ni kwamba hakuna njia ya mkato katika mafanikio. Msemo huu una maana sana hasa katika ulimwengu wa michezo.

Wanamichezo wangependa kuvaa medali kwa juhudi kidogo na pia viongozi wa michezo wangependa wawe na timu zenye mafanikio wakati mwingine kuzidi gharama waliyoingiza katika timu zao. Hakuna njia ya mkato ya mafanikio katika michezo na hakuna bei iliyobandikwa ya kuuza mafanikio.

Mafanikio katika michezo ni sehemu ya mpango wa maendeleo endelevu. Mafanikio si lelemama.

Kufuatia kutolewa kwa timu ya Yanga katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hali kadhalika kutolewa kwa Azam FC na Kipanga FC katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kumeacha minong’ono na hata malalamiko miongoni mwa wafuatiliaji wa mchezo wa soka. Wakati Azam na Kipanga hazitajwi sana, ni Yanga ambayo imetajwa kwa kuonekana imefeli‚ sana kwa kutolewa katika raundi ya kwanza na Al-Hilal Omdurman ya Sudan.

Watanzania hawa wanaona kama kutolewa au kufungwa na klabu ya Sudan ni jambo la fedhea.Watu hawaoni mambo chanya katika ushiriki wa timu zetu pindi zinapokuwa hazijakidhi, ‘matarajio,’ ya wapenzi wao. Tunalaumu bila kuangalia mambo chanya katika kukutana na walio bora. Wakati mwingine masononeko ya mashabiki huwa ni matokeo ya matarajio ya kukamua maziwa mengi kutoka ng’ombe aliyekonda.

Taifa la Sudan inakotokea Al-Hilal iliyocheza na Yanga liliunda chama cha mpira wa miguu mwaka 1936 na kujiunga na FIFA mwaka 1948. Sudan ilikuwa mmoja wa waanzilishi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na kuwa mwenyeji wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1957 ambako walichukua nafasi ya tatu na kurudia tena mwaka 1959 na pia nafasi ya wameshinda Kombe la Mataifa ya Afrrika mwaka 1970.

Columnist: Mwanaspoti