Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tusidanganyane, hakuna hatua tulizopiga katika Soka

Makala Yanga Tusidanganyane, hakuna hatua tulizopiga katika Soka

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sikilizeni Wachambuzi wa Soka, tufike hatua tuseme kuwa Vilabu vyetu ni Masikini haviwezi kushindana kimataifa katika level tunazo zitaka, Wala mistake kusema oooh Kuna hatua tumezipiga hapa ,Kucheza Ugenini dhidi ya timu za North afrika zinahitaji Quality only wala hakuna sijui wachezaji wafupi hapana.

TP Mazembe ya kina Samatha, Ulimwengu, Raford Kalaba, Kabaka Chongo ,Rogger Assale, Frimpong, Mputu walikuwa na quality yenye uwiano.

Shida sisi tuna Quality ambayo haina uwiano, una Diarra, Djuma, Aziz, Mayele wengine ni Average player.

Una Manula, Kapombe, Mohamed Hussein, Onyango wengine ni Average playe ndo utarajie kuchukua Ubingwa wa Afrika.

Kwa hiyo hiyo hoja ya oooh wamejitahidi tusiipe nafasi tuseme bado tunahitaji uwekezaji mkubwa katika timu zetu na ligi yetu kwa ujumla.

Tunafungwa kwa sababu timu hazina uwezo wa kushindana katika level hiyo, kumfunga Mazembe siyo kazi rahisi labda itokee tuu kama Vipers walivyo pata Bahati hiyo.

Hoja inayo paswa kujadiliwa kwa kina ni kuhakikisha Vilabu vinakuwa na Quality, T.F.F na Bodi ya Ligi toeni vipingamizi vya wachezaji wa kigeni, Wekeni kigezo cha timu zinazo shiriki ligi kuu kusajili wachezaji wa kigeni 18 ili muweze kuvisaidia Vilabu vyetu kushindana, Inapaswa level ya kina Aziz Ki wawe pale Yanga hata 8 ndiyo timu itafanya vizuri.

Kocha Pitso aliwahi kusema;

"The simple truth is that many North African clubs possess sizeable budgets, allowing for the construction of infrastructure and better player acquisition,akimaanisha "Kiukweli timu za afrika ya kaskazini zina uchumi mzuri unaowawezesha kujenga miundo mbinu bora na kupata wachezaji wazuri"

Sasa tuendelee kudanganya etii oooh tunataka nusu fainali, kuvunja hiyo layer inahitaji uchumi, tuwe tayari kuwekeza kwa wachezaji bora siyo hawa akina Morrison, Wachezaji haswa wa daraja la juu.

Columnist: www.tanzaniaweb.live