Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tunapongeza safari za ndege Tanzania, Kenya kurejea

F8bc282f729777d116166ac26f3a6a1c Tunapongeza safari za ndege Tanzania, Kenya kurejea

Tue, 22 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HATIMAYE safari za ndege kati ya Tanzania na Kenya zimerejea upya. Safari hizo zimeanza baada ya ndege za Kenya kuanza safari zake za kila siku jijini Dar es Salaam jana.

Awali, safari za ndege baina ya nchi hizo mbili, zilisimama kwa muda baada ya Kenya kutoa orodha ya mashirika ya ndege yanayoruhusiwa kutua nchini humo bila ya kuiweka Tanzania, katika kile ilichoelezwa ni mikakati yake ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vua corona.

Siku chache baadae Tanzania nayo ilichukuwa hatua kama hiyo kwa Kenya. Wiki iliyopita Tanzania iliondoa marufuku dhidi ya safari za ndege za Kenya nchini, ikiwa ni siku moja tu baada ya Kenya kuwaruhusu raia wa Tanzania kuingia Kenya bila kutakiwa kukaa karantini ya lazima ya siku 14 kwa ajili ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari, kwa sasa mambo ni shwari baada ya Tanzania na Kenya kukubaliana safari za ndege kuanza rasmi.

Kwa upande wa Tanzania, ndege za mashirika ya hapa nchini ikiwamo Precision Air zimeishaanza safari zake tangu juzi, huku ndege nyingine zikitarajia kwenda nchini humo hivi karibuni kama ilivyokuwa awali.

Tunapongeza hatua ya kuanza tena safari hizo, tukiamini itasaidia kukuza ushirikiano wa kibiashara, pamoja na kukuza utalii na biashara baina ya mataifa hayo jirani.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Kenya, mwaka jana thamani ya biashara ya nje kutoka Kenya kwenda Tanzania ilikuwa kwa wastani wa dola za Marekani milioni 336, huku ikiingiza bidhaa za dola za Marekani milioni 275.

Hatua hiyo pia itarahisisha usafirishaji bidhaa na kuongeza fursa za upatikanaji wa masoko na utalii.

Columnist: habarileo.co.tz