Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tunahitaji tahasusi ya kilimo biashara, ujasiriamali, viwanda

C9eeee567a53015e917c59945ef15636.png Tunahitaji tahasusi ya kilimo biashara, ujasiriamali, viwanda

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MACHI 29 mwaka huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alitangaza kuwa, serikali inaanzisha tahasusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato cha tano mwaka 2021.

Tahasusi hizo ni Physics, Mathematics na Computer Studies (PMC); Kiswahili, French, Chinese (KFC); Kiswahili, English, Chinese (KEC); Physical Education, Biology, Fine Art (PBF) na Physical Education, Geography, Economics (PGE).

Naipongeza serikali kwa kuongeza wigo wa tahasusi kwa kuongeza idadi ya masomo kwenye mtaala wa elimu ya juu ya sekondari.

Tahahusi zilizopo tangu miaka ya nyuma ni pamoja na PCM (Physics, Chemistry, Mathematics), CBG (Chemistry, Biology, Geography), HGL (History, Geography, Language).

Wanafunzi wa kidato cha tano na sita pia wanasoma HGE (History, Geography, Economics), HKL (History, Kiswahili, Language, PCB (Physics, Chemistry, Biology) na ECA (Economics, Commerce, Accounts), KLF (Kiswahili, Language, French), HKF (History, Kiswahili, French).

Pamoja na nia njema ya serikali, ni mtazamo wangu kuwa kuanzishwa kwa tahasusi mpya hakukuzingatia vipaumbele vya sasa katika ujenzi wa uchumi wa nchi yetu na kasi inayohitajika.

Kwa mfano, Serikali ya Awamu ya Tano inahimiza ujenzi wa Tanzania ya viwanda lakini hakuna tahasusi hata moja yenye somo la maendeleo ya viwanda (industrialization).

Serikali pia inahimiza mapinduzi ya kilimo kupitia kilimo biashara (Angroeco-nomics) lakini inasikitisha hakuna tahasusi hata moja yenye somo la kilimo. Unapataje mapinduzi ya kilimo wakati wanafunzi shule za msingi na sekondari hawafundishwi kilimo cha kisasa cha biashara?.

Kama kilimo biashara kikifundishwa kidato cha tano na sita itasaidia kubadili mtazamo wa vijana kwa sababu wataona faida ya kulima badala ya kukaa bure mijini au mitaani.

Si hivyo tu, Watanzania wanahimizwa kuzitumia fursa kujiajiri lakini hakuna tahasusi hata moja yenye somo la ujasiriamali(Entrepr eneurship).

Wahitimu wengi wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita wameingia kwenye ujasiriamali lakini hawana uelewa kuhusu mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na utafiti, masoko, mitaji, utunzaji hesabu, ushindani kwenye masomo, ufungashaji bidhaa, ubunifu, mamlaka za udhibiti, sheria za biashara na kadhalika.

Tubadili mitazamo kuhusu mfumo wetu wa elimu ili mitaala izingatie mahitaji halisi ya sasa. Tuache kuzingatia masomo yanayomhitaji mwanafunzi akariri tu ili afaulu mitihani na kupata cheti kizuri kisichomsaidia kwenye maisha halisi baada ya kuhitimu.

Nashauri mamlaka kila zinazopofanya mabadiliko ya tahasusi zizingatie vipaumbele vya nchi na mahitaji ya wakati huo. Kwa mfano, kuna ubaya gani kwa tahasusi ya AEI (Angroeconomics, Entrepreneurship, Industrialization)?

Mhitimu wa tahasusi hii atakuwa na wigo mpana wa kuamua ajiajiri kwenye kilimo biashara, au ujasiriamali, au kuanzisha kiwanda badala ya kusubiri kuajiriwa.

Columnist: www.habarileo.co.tz