Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tunafanyaje kuendeleza uwepo wa wanawake katika sayansi?

03b23f716a675331dc3412c92e6914a6 Tunafanyaje kuendeleza uwepo wa wanawake katika sayansi?

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

FEBRUARI 11 kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi. Lengo la siku hii ambayo iliadhimishwa jana ni kuweka fursa kwa wote kuchukua msimamo kwa ajili ya wasichana na wanawake katika sekta hii muhimu.

Lakini pia siku hii inaainisha umuhimu wa sayansi katika jamii na kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya sayansi, amani na maendeleo. Kwa Tanzania ambako bado masomo na shughuli za kisayansi bado zimetaliwa na wanaume, jana ilikuwa siku muhimu sana katika kuwahamasisha wasichana na wanawake kujikita katika sayansi.

Katika kuadhimisha siku hii iliyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2015, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (Unesco) limesema wasichana wanaendelea kukumbwa na ubaguzi, vikwazo vya kijamii na kitamaduni ambavyo vinawazuia kupata elimu na fedha za kufanya tafiti.

Kwamba wanaazuia pia kuingia katika kazi zitokanazo na masomo ya sayansi na hivyo kuwakwamisha kufikia uwezo wao kikamilifu.

Unesco linasema idadi ya wanawake katika tafiti za sayansi na uamuzi bado ni ndogo sana. Hali hii inaleta kikwazo kikubwa katika juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Kimsingi, taswira hii inapaswa kubadilika na hii itawezekana iwapo wasichana na wanawake watapata fursa ikiwa ni pamoja na kundi hili lipewe motisha ikiwemo upndeleo malaamu ili kuhakikisha kwamba sekta ya sayansi inawakilishwa na wanawake vilivyo.

Swali la kujiuliza: Je, hali ya Tanzania na Afrika Mashariki ikoje? Je, jamii inafanya nini kuendeleza uwepo wa wasichana na wanawake katika sayansi?

Ujuzi katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati unachagiza ubunifu na ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Guterres katika ujumbe wa siku hii anasema kwamba wanawake na wasichana ni wa muhimu katika maeneo yote haya, lakini bado uwakilishi wao ni mdogo. Anaongeza: “misimamo ya kijinsia, ukosefu wa watu ambao ni mifano inayoonekana na sera na mazingira yasiyofaa au hata ya uadui vinaweza kuwazuia kuingia katika kazi hizi.”

Anasisitiza kwamba dunia haiwezi kumudu kukosa mchango wa nusu ya watu wote duniani, na hivyo juhudi za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na vikwazo hivi ikiwa ni pamoja na hisia zisizofaa kuhusu uwezo wa wasichana.

Anazidi kusema kwamba ni lazima,“tuchagize fursa za kupata elimu kwa wanawake na wasichana, hususan maeneo ya vijijini.”

Katibu Mkuu huyo anahimiza juhudi zaidi za kubadili utamaduni wa mahali pa kazi ili wasichana ambao wanapenda kuwa wanasayansi, wahandisi na wataalamu wa hisabati waweze kufurahia na kutimiza ndoto zao za kazi katika nyanja hizi.

Anatoa mwito wa kuhakikisha kwamba kila msichana, kila mahali ana fursa ya kutimiza ndoto zake, kukuza uwezo wake na kuchangia katika mustakabali endelevu kwa wote.

Kwa ujumla siku hii inasisitiza kutoa fursa kwa kundi la wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao na haja ya kushirikisha jamii katika mjadala wa masuala ya kisayansi yanayoibuka na umuhimu wake katika maisha ya watu ya kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), Bibi Audrey Azoulay anabainisha kuwa lengo la siku hiyo iliyoadhimishwa jana ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kila wakati kuhusu umuhimu wa wanawake na wasichana katika maeneo yote haya za maendeleo ya sayansi.

Pia anasema siku hii inahimiza jukumu kubwa walilonalo wanasayansi wote katika kuielewa dunia yetu na changamoto zake katika kuzifanya jamii hizo kuwa endelevu.

Hadi sasa, sayansi inaendelea kuwa nguzo kuu ya Ajenda ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu; Ajenda ya Addis Ababa ya Kuchukua Hatua; Mkakati wa Kupunguza Hatari za Majanga wa Sendai; na Makubaliano ya Paris ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Dunia inakabiliwa na migogoro mingi. Lakini hii pia ni zama zenye fursa, ambapo mafanikio makubwa yanawezekana, shukrani kwa sayansi, teknolojia na ubunifu.

Kufika kwa huduma za simu za mkononi na kuhamisha fedha kupitia simu hizo ni moja ya mifano. Sayansi imepanua shughuli za benki, mawasiliano na uwezekano wa kufikia watu majumbani, ikiwa ni pamoja na maeneo ya ndani zaidi.

Maendeleo makubwa ya sayansi ni muhimu ikiwa yatasaidia mchakato wa kukuza na kudumisha umoja na mafungamano ya kijamii; kanuni maadili na utu wema; siasa shirikishi pamoja na haki.

Katika ulimwengu huu ambamo watu wanathamini sana takwimu, kuna haja ya kuhakikisha kwamba, utu, heshima na haki msingi za binadamu zinaheshimiwa.

Ikiwa mitandao ya kijamii itatumika kama daraja na matumaini ya kuwakutanisha watu, basi hapo itakuwa imetekeleza dhamana na wajibu wa kujenga jumuiya inayoheshimiana na kuthaminiana.

Matumizi ya teknolojia ya mfumowa wa utambuzo (Artificial Intelligence) yanaendelea kuleta mageuzi makubwa katika ulimwengu wa kazi na mahali wanapoishi watu! Mabadiliko haya ni makubwa, yanapaswa kuongozwa na kusimamiwa na sheria, kanuni maadili na utu wema.

Maendeleo ya sayansi yanachangia kwa kiasi kikubwa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi, lakini hayana budi kufumbatwa katika utu na heshima ya binadamu.

Makubaliano haya yote yanatoa maono mapya ya amani na ustawi wa dunia, li kuwezesha kuwa na jamii yenye kujenga na kubadilishana maarifa, kuendeleza uvumbuzi na ubunifu kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa maendeleo endelevu naya pamoja kwa siku zijazo.

Ili kufanikisha hili, kunahitajika kutoa fursa kwa wasichana na upanuzi zaidi wa tasnia ya sayansi kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa mahusiano chanya baina ya sayansi na jamii.

Hii ndiyo sababu kuu kwa nini Vituo na Makumbusho ya Sayansi ni muhimu kwa ajili ya kujenga uwezo, kutetea na kupeleka ujumbe kuhusu umuhimu wa sayansi katika maendeleo endelevu.

Vituo na Makumbusho ya Sayansi kwa pamoja vina jukumu kubwa la kulea udadisi wa wasichana na wanawake, kama maabara hai ya ubunifu ili kuchochea utafiti na kuweza kuisaidia jamii hii kukabiliana na changamoto zake.

Katika zama hizi za dijitali, wakati ambao tunahitaji jitihada za ubunifu kukuza masomo ya sayansi nje ya madarasa, vituo na makumbusho ya sayansi ni maeneo muhimu katika kusaidia hilo. Vinatoa njia sahihi ya kuhamasisha watoto hususani wasichana kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza uwezo na ufanisi wa kisayansi.

Novemba 2015, Unesco iliridhia pendekezo la dunia la kutunza na kuendeleza makumbusho pamoja na machapisho yake, nyaraka zake zingine na wajibu wake mbele ya jamii ili kuimarisha dhamira ya Unesco ya kuhamamisha makumbusho kuwa nyenzo muhimu ya amani na maendeleo endelevu.

Vituo na Makumbusho ya Sayansi ni majukwaa muhimu kwa ajili ya mazungumzo ili kuweza kuelewa na kuwa na uwezo wa kupambana na masuala mbalimbali.

Vinatoa cheche za furaha na maajabu yanayohamasisha wageni mbalimbali bila kujali umri wala asili, kwa kutoa uzoefu unaowaleta pamoja wanawake na wanaume wenye maadili yanayofanana.

0685 666964 au [email protected]

Columnist: habarileo.co.tz