Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Trippier vs De Bruyne, Mtenje vs Bangala

Trippier Vs KDB Trippier vs De Bruyne

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Arsenal kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kukusanya pointi tisa ilizozipata katika mechi tatu mfululizo za mashindano hayo.

Arsenal ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya timu ya Crystal Palace, Agosti 5 na baadaye ikashinda kwa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Leicester City kisha ikapata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya FC Bournemouth ambao iliupata Jumamosi waiki iliyopita ikiwa ugenini.

Ni matokeo ambayo yanawafanya mashabiki wa timu hiyo kutembea kifua mbele kwa sasa kwani ndiyo timu pekee hadi sasa haijapata matokeo ya sare katika michezo mitatu na imejikusanyia pointi tisa ikipigwa na ‘baridi’ kileleni mwa msimamo.

Mbali na matokeo hayo ambayo bila shaka mashabiki wa Arsenal yamewapa furaha kubwa, ligi hiyo ilikuwa na mechi mbalimbali ambazo kama kawaida kulikuwa na matukio tofauti ya kutatanisha na yanayohitaji kutolewa ufafanuzi.

TUKIO

Moja ya matukio makubwa katika mechi za wikiendi iliyopita ni kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa mchezaji wa Newcastle United, Kieran Trippier na mwamuzi Jarred Gillett ambaye ni raia wa kwanza wa Australia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya England. Mwamuzi huyo alianza kuchezesha mechi Septemba, mwaka jana kati ya Watford dhidi ya Newcastle.

Gillett alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Tripper kwa kumchezea rafu kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne.

Hata hivyo, Gillett ambaye alisaidiwa na Lee Betts, Ian Hussin na mwamuzi wa akiba Tony Harrington, alibadili uamuzi huo na kumpa onyo la kadi ya njano Trippier baada ya kwenda kujiridhisha kwenye televisheni ya pembeni ya uwanja iliyounganishwa na VAR.

Uamuzi huo ulionekana kuwafikirisha mashabiki wa soka wengi na hata baadhi ya wachambuzi wa mchezo huo.

Kilichotokea ni kwamba baada ya Newcastle United kufanya shambulizi wachezaji wa Manchester City walifanya shambulizi la haraka (counter attack) na Trippier aliona njia pekee ya kuzuia wasipate madhara katika shambulizi hilo ni kufanya ‘slide tackle’ na kuonekana kumgonga kwenye kifundo cha mguu De Bruyne akaangusha chini.

Uamuzi huo ulipongezwa na mshambuliaji wa zamani wa England, Gary Lineker, lakini Jamie Carragher alipinga uamuzi huo na kusema Trippier alitakiwa kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Ukiachana na tukio hilo, hapa nyumbani kulikuwa na tukio ambalo mpaka sasa bado linaendelea kuibua mijadala kwa wadau wa soka. Tukio hilo linamhusisha Mtenje Albano wa Coastal Union dhidi ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Yannick Bangala wa Yanga.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid - Arusha, Albano alimchezea rafu Bangala ambapo kabla ya mwamuzi kutoa adhabu Bangala alikwenda kurudisha kwa kumsukuma Albano ambaye alianguka chini.

Ni tukio ambalo lliwafanya mashabiki wengi wa soka waliofuatilia mchezo huo kubaki na mitazamo tofauti huku wengine wakimrushia lawama mwamuzi kwa kutompa kadi nyekundu Albano na wapo pia waliolaumu kitendo cha mwamuzi kumpa kadi ya njano Bangala.

SHERIA ZINASEMAJE

Trippier vs De Bruyne

Ni wazi kwamba Trippier alifanya faulo ambayo ilistahili onyo kwa mujibu wa sheria namba 12 ya Fifa na bodi ya kutunga sheria za soka (Ifab).

Mwamuzi Gillett hakuwa katika eneo sahihi wakati tukio linatokea ili kuliona moja kwa moja kuwa Trippier alimkwatua kwa nyuma De Bruyne na kumuadhibu kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Hata hivyo, picha za marejeo zilionyesha kuwa Trippier alifanya ‘slide tackle’ ambayo haikuwa na madhara makubwa kwa De Bruyne zaidi ya kumzuia kwenda mbele.

Hivyo kitendo cha mwamuzi kuifuta kadi nyekundu ya moja kwa moja ilikuwa sahihi pamoja na uwepo wa maoni au mitazamo tofauti kuhusiana na uamuzi huo.

Mtenje vs Bangala

Katika tukio lililowahusisha mastaa hawa baadhi ya mashabiki walitarajia mwamuzi angemwadhibu kwa kadi nyekundu Mtenje kutokana na mchezo wa rafu aliyoifanya kwa Bangala kwa mujibu wa sheria namba 12 ya Fifa na Ifab.

Hata hivyo, kitendo cha mwamuzi huyo kutoa kadi ya njano kwa Mtenje na Bangala ni kwa sababu kubwa mbili.

Ni wazi kuwa Mtenje alidhamiria kucheza rafu mbaya kwa Bangala ambapo kama angefanikiwa kufikishia kwanja alilokuwa amedhamiria ni wazi kwamba angeweza kumuumiza vibaya na kuhatarisha usalama wa mwenzake ikiwamo taaluma ya soka anayoitumikia ili kujipatia kipato.

Kwa upande wa Bangala alipaswa kupewa kadi ya njano (kama mwamuzi alivyofanya) na hiyo ilitokana na kitendo cha kumvamia Mtenje.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz