Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tofauti ya wageni na wazawa katika vilabu vyetu ni Mbingu na Ardhi

Aziz Ki X Mayele Tofauti ya wageni na wazawa katika vilabu vyetu ni Mbingu na Ardhi

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimeona kikaratasi kinatembea kwa mara nyingine, kiliwahi kutembea pia kikionesha mishahara ya wachezaji wa Yanga, mie naichukulia kama mfano japo sina uhakika nayo sana haswa chanzo chake na chanzo rasmi kutokua tayari kutoa taarifa za watumishi wao.

Kushinda Battle ya kibiashara ni sanaa, kushinda na kupata matokeo chanya ya makubaliano ya biashara ni ushindi unatokana na kujua namna ya kuielezea Thamani yako kama uwekezaji na Return Yako kama Utapewa unachotaka. Nimeichukulia kwa Mtu binafsi na Taasisi.

Wachezaji wetu na wasimamizi wao kwa asilimia kubwa huwa wanashindwa hivi vitu wakishafika kwenye meza ya Majadiliano. Mbali na wazawa kudharauliwa na kuchukuliwa kama watu wanaosaidiwa na mameneja nao wapo kundi moja nao wanasaidiwa vile vile (Asilimia kubwa)

Nitakupa Mkasa wa Meneja wa zamani wa winga na Meneja wa Winga, kwa mujibu wa maongezi yangu na Meneja wa Winga eti klabu ilikataa kumpa mkataba winga kisa uongozi hauna mahusiano mazuri na meneja wake wa zamani. Hili ni Tatizo kubwa, wachezaji wamekua hawana sauti sababu ya uoga na hii ndio imepelekea mishahara mbuzi. Mameneja wanaenda kishkaji na deal zinaishia Baa.

Natamani watu waelewe uzito wa hiki nilichokiongea lah sivyo wachezaji wazawa hawatapata mishahara minono hadi hiki kizazi cha kina Meneja wa Winga kifutike sababu kwa asilimia kubwa kinaharibu meza ya makubalino. “Negotiation should not be influenced by any other factor than business” Japo Mahusiano ni muhimu yatunzwe.

Tuamue sasa kufanya biashara, tuamue sasa kuwapa wachezaji jeuri juu ya vipaji vyao linapokuja suala la maslahi ya vipaji vyao na sio kutembea kwa huruma matokeo yake unalipwa Milioni 3 kisha makato ni nusu ya pesa kulipa fadhila. Hii ndio sababu inapelekea wachezaji wa Tanzania kushindwa kuishi kama mastaa wengine. Leo Sure Boy hawezi kukanyaga anga za Jay Melody licha ya kucheza Soka kwa muda mrefu sasa.

Columnist: www.tanzaniaweb.live