Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Thadei Ole Mushi; The Hero of Freethinking!

Thadei Ole Mushi Thadei Ole Mushi enzi za uhai wake.

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Luqman Maloto

Ulimwengu ni jukwaa la mateso kwa watu huru kifikra. Wenye kutumia akili zao kupokea, kutafsiri na kujenga hoja. Wanaounda mitazamo na misimamo baada ya kujiridhisha kwa tafakuri binafsi.

"The essence of the independent mind lies not in what it thinks, but in how it thinks." - "Msingi wa fikra huru hauegemei katika nini unafikiri, bali kwa jinsi unavyofikiri." Ndivyo alisema mwandishi wa UK, Chris Hitchens.

Watu wenye kujitegemea kifikra na kuamua kufuata jambo kwa utashi wa fikra binafsi, mara nyingi hugeuka wapweke. Upo wakati utafikiri tofauti na wengine. Utajikuta upo peke yako. Si ajabu ukazodolewa, hivyo kuifanya dunia kuwa ngumu upande wako.

Dunia ni nyepesi kwa wafuata mkumbo. Upepo unapovuma na wao wanaunga. Hawaumizi kichwa, wakisikia mayowe wanafuata. Akisema fulani, naye anaamini hata kama huyo msemaji ni Kizabizabina.

Thadei Ole Mushi. Mwalimu kitaaluma. Mwandishi na mmoja wa wajenga hoja huru ninaowafahamu na kuwatambua. Soma makala za Thadei. Andiko kwa andiko. Posti zake. Alivyojenga hoja na misingi aliyosimamia. Thadei ni mantiki ya fikra huru.

Hakuona aibu kujisema yeye ni kada wa CCM. Hata sare za chama alivaa. Shughuli za CCM alishiriki waziwazi. Kisha, ungemsoma Thadei akiikosoa serikali, vilevile chama chake. Ni kwa sababu msingi wa fikra zake, haukuegemea alichofikiri, bali jinsi alivyofikiri.

Tembelea akaunti zake, soma posti kwa posti. Kuna mahali aliandika, watu kwa wingi wao, walimpongeza. Kwingine alijenga hoja, watu kwa wingi kabisa walimshambulia, walimpinga na kumpa majina mabaya. Hiyo ndiyo gharama ya kuushughulisha ubongo kwa utofauti.

Abraham Lincoln, alifundisha kusimamia unachokiamini, hata kama kila mtu anafuata mkumbo. Ni somo zuri, ila linaweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Fikiria unauona ukweli ambao kila mtu hauoni. Halafu wewe mwenye ukweli, unaitwa majina mabaya.

Nilifahamu Thadei alikuwa katika hali ya kupigania maisha yake kutokana na maradhi ya moyo. Nilijua angenyanyuka akiwa imara. Leo nikapokea habari kuwa Thadei amepumzika. Sikuamini. Binadamu hatujawahi kukikubali kifo.

Kwangu, Thadei ni shujaa wa ufikiri huru. He's a freethinking hero!

Ndimi Luqman MALOTO

Columnist: Luqman Maloto