Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tanzania iendelee kuwa mfano Uchaguzi Huru na Amani EAC

FSD Tanzania iendelee kuwa mfano Uchaguzi Huru na Amani EAC

Tue, 27 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KESHO watanzania wanapiga kura kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano katika ngazi za uongozi za urais, ubunge na udiwani.

Katika chaguzi zote zilizoshirikisha wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa, wagombea na wananchi wamekuwa wakishiriki kikamilifu na hatimaye kutangazwa wagombea na baadhi ya changamoto zilizojitokeza zimekuwa zikifanyiwa na kazi na kila mmoja kuridhika.

Katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka huu Burundi imefanya uchaguzi wake na kukamilika kwa amani na utulivu, jambo lililoonesha ukomavu wa kisiasa kwa wananchi wa nchi hiyo ambayo kwa miaka kadhaa walikuwa wakijikuta wanaingia katika ghasia na vita mara baada ya uchaguzi.

Tanzania ikielezwa kuwa na mchango mkubwa katika upatikanaji wa amani hususan kupitia kwa mpatanishi wa Burundi kwa miaka mingi Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa ni dhahiri Tanzania inajivunia kuwezesha amani kulikowezesha Rais Evarist Ndayishimiye kuchaguliwa.

Tanzania ambayo ni kitovu cha amani na utulivu EAC, kwa mara nyingine inaingia kwenye uchaguzi mkuu ikitangulia nchi za Uganda na Kenya wanaotarajia kufanya chaguzi zao kuu mwaka 2021 na Sudan kusini ikipanga kufanya uchaguzi mwaka 2022.

Kwa baadhi ya nchi ambazo zinajiandaa katika kufanya chaguzi zao ni dhahiri wanajifunza kwa jinsi Tanzania ilivyofanya mchakato huu kwa amani na utulivu ili kuimarisha amani kwenye ukanda wa EAC.

Kwa uchaguzi huu wenye wagombea katika ngazi ya urais 15 ni nafasi nyingine ya watanzania kudhihirisha kuwa kisiwa cha amani kwa kutokubali kushawishika au kuingiliwa na taifa lolote katika kufanya chaguzi hizi.

Kwa kile kilichoanzishwa kuhakikisha kunakuwa na amani kwenye kampeni zinazomalizika leo kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusimamia sheria na taratibu kwa nguvu zote na kuhakikisha kunakuwa na amani na utulivu katika kampeni zote hakika watanzania hawatashindwa kwenye siku ya uchaguzi.

Ni dhahiri kuwa, Watanzania wamedhamiria kuwepo kwa amani kwani hata wachache waliojaribu kwenda kinyume cha sheria na taratibu wakati wa kampeni walichukuliwa hatua na kupewa adhabu ambazo walikubali na kutumikia bila kuleta uhasama.

Kama ilivyokuwa miaka mingine, ni dhahiri Watanzania watatumia siku ya kesho kupata viongozi na si kusababisha au kuanzisha vurugu kwa kufuata sheria na pale ambazo kuna changamoto ni vema kutatuliwa kwa pamoja kwani hakuna tatizo lisilo na suluhisho.

Ni vema kwa kufuata sheria na taratibu, kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika siku hii ambao ni mapumziko kisha kurejea nyumbani kusubiri mamlaka husika kutangaza washindi.

Kitendo cha kupewa mamlaka na nchi kusimamia uchaguzi ni vema kuwa na imani na wasimamizi wote kuwa watatangaza wagombea walioshinda kufuata sheria na taratibu na kamwe tusikubali kuchochewa na watu wachache wanaotaka vurugu kwa maslahi.

Kumalizika kwa uchaguzi huu wa amani na utulivu, itadhihirisha Tanzania kuendelea kuwa mfano kwa nchi nyingine za EAC zinazotarajia kufanya chaguzi, kuwa kamwe wakati wa uchaguzi sio kuanzisha vurugu bali kila mmoja kutumia vema haki yake ya kidemokrasia.

Kila la heri kwa watanzania wote katika kupata viongozi watakaoongoza kwa muda huu na kamwe yeyote atakayejaribu kusababisha vurugu ni vema kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa nchi zote za EAC.

Columnist: habarileo.co.tz