Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tangulia JPM, daima utabaki milele vichwani mwetu

MAGUFULI 13?fit=700%2C394&ssl=1 Tangulia JPM, daima utabaki milele vichwani mwetu

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Baada ya kutangazwa kifo chake Machi 17, mwaka huu, nchi ilizizima na ilikuwa ukitazama mwonekano wa watu katika maeneo tofauti tangu siku hiyo walio wengi wana simanzi usoni.

Imetia fora, kutokana na tangu ratiba ya mazishi ilipoanza jijini Dar es Salaam, Dodoma, visiwani Zanzibar na Mwanza, idadi ya waliojitokeza kuuaga mwili wake, imepindukia.

Ushiriki wa viongozi kutoka mataifa mbalimbali hususan barani Afrika, mabalozi na taasisi za kimataifa kunadhihirisha upendo uliopo kati ya nchi na mwananchi mmoja mmoja kwa kiongozi wao.

Watanzania kuanzia viongozi ngazi ya mtaa, kata, kijiji, tarafa, wameshiriki kumwomboleza kiongozi wao, iwe kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au kushuhudia ana kwa ana, inaweza kuwa kumbukumbu kwa vizazi na vizazi.

Pengine, inatokana na tukio hili kuwa la kwanza kutokea nchini, Rais kufariki dunia akiwa madarakani na kusababisha simanzi kwa Watanzania.

Matarajio ahadi na namna ya uendeshaji serikali yake ikiwamo utekelezaji na usimamizi wa ana kwa ana wa shughuli zinazogusa jamii, ikawa kumbukumbu inayobeba tukio hili kuongeza majonzi kwa Watanzania.

Lakini, uongozi wake Hayati Magufuli, ni alama na umetoa funzo kwa kila mmoja maishani mwake.

Pale walipohojiwa baadhi ya wananchi ikiwamo wajasiriamali, wamachinga, watumishi kupitia vyombo vya habari, wanamweleza kuwa ni kati ya viongozi wakuu, wananchi, walitoa elimu ya namna ya kuishi kwa kufuata kanuni na kuwa na nidhamu ya kila kitu hasa pesa.

Binadamu yeyote anaweza kufanikiwa, iwapo anakuwa na vipaumbele vyake, licha ya kila mwanadamu kuwa na mahitaji lukuki, kwa kuwa na bajeti maalumu inayoendana na kipato chake.

Wanasema kuwa, mfumo wa kuishi kwa kufanya kazi zaidi, kupitia falsafa yake ya hapa kazi tu, kulitoa morali ya kila mmoja kujishughulisha.

Kwamba palipo na fursa pakitumika ipasavyo kila mmoja atapata riziki yake, badala ya kusubiri cha kupewa na mtu.

Dhana hiyo aliyoijenga, walioitafsiri kwa mtazamo chanya na kuitumia, ndio hao kwa kiwango kikubwa ambao wanaonekana kwenye msafara wa kusindikiza mwili wa Hayati Magufuli, kumsindikiza katika safari yake ya mwisho duniani.

Mtindo wake wa kupita katika miradi tofauti, kuruhusu wananchi kuelezea kero zao awapo kwenye ziara zake, huku akiwataka viongozi wa maeneo husika kutoa majibu papo hapo, kumewaachia kumbukumbu wengi.

Hii pia inawakumbusha watumishi wa umma kuutumikia umma, ili kutatua matatizo yaliyopo ndani ya jamii kupitia elimu waliyoipata darasani.

Katika jamii yapo masuala muhimu ya kutiliwa mkazo na ndiyo kero katika jamii ambayo umma unasubiri serikali kuwatatulia.

Mathalani, suala la maji, elimu, afya, barabara ni kati ya mahitaji ya binadamu hususan nchi zinazoendelea yanayohitaji kutatuliwa.

Huduma hizo kwa kiongozi yeyote ambaye anapata fursa kuutumikia umma zikipatiwa ufumbuzi ataacha alama ya kumbukumbu.

Katika hilo, JPM hatua ya kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, kumeokoa kundi la mabinti wadogo ambao walishindwa kufikia hatua hii kutokana na uchumi duni wa wazazi wao huku baadhi ya mila na desturi zikiwakandamiza.

Yapo, mengi lakini suala la elimu bure, kuongeza bajeti ya afya kumeokoa maisha ya kinamama na watoto kutokana na huduma kuboreshwa.

Buriani mpendwa wetu JPM.

   

Columnist: ippmedia.com