Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Tamaa bila mipango ni ujinga

Fei X Case Tamaa bila mipango ni Ujinga

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

️Hii leo ukitaja jina Casemiro kila mtu atajua umemaanisha "A world class player " "mchezaji wa daraja la dunia" huyu ni miongoni mwa wachezaji wanaokubalika na watu wengi kutokana na aina yake ya uchezaji.

Umaarufu wa Casemiro umezalishwa na jina Real Madrid, wakati yuko Sau Paulo, hakuna aliyetambua jina la huyu mtu.

Real madrid imempa heshima ya kipekee Casemiro, tukumbuke pale Santiago Bernabeu, alidumu kipindi cha miaka tisa na alifanikiwa kushinda Vikombe mbali mbali ikiwemo UEFA champions league (5) La liga (3) na vingine vingi.

katika kipindi hicho cha mafanikio Casemiro alikuwa ni mchezaji muhimu, panga pangua.

Cha kushangaza Casemiro, ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanalipwa pesa kidogo na Real.....malipo yake kwa wiki ilikuwa ni €160,000 kwa wiki huyu jamaa alizidiwa na Isco €24,5000,Luca Jovic €180,000 hadi Eder Militao na Ferlan Mendy wote walikuwa juu yake €180,000.

Lakini Casemiro aliendelea kuheshimu mkataba wake na kuzidi kukitifua kwani alijua fika Real Madrid wanamtambulisha duniani na pesa itakuja.

Muda ulipofika wa kutaka hela kubwa alimwambia wakala wake Joseph Lee,azungumze na vilabu vya Man utd na Inter Milan ili aweze kujinga navyo tena akaenda mbali zaidi na kuahidi kuwa atamaliza kabisa tatizo la Manchester United pale kati kati ya uwanja.

Baada ya hapo akawaaga wachezaji wenzake wa Real na Mr Perez,kisha akaondoka kwa amani...na hivi sasa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa hela ndefu na Manchester United €350,000 kwa wiki.

Ndugu Yangu Fei hata kama Yanga walikuwa wanakulipa Milioni 4 hukutakiwa kuondoka vile...Yanga ndio Timu iliyo kutambulisha mjini na kukupa madili kibao.

Fei ungetulia na kusubiri wakati sahihi wa kuvuna hela...ona sasa Huchezi mpira na umri unasogea,amani ya moyo umeipoteza na unazidi kupoteza mashabiki zako, na wapenzi wa mambo yako...Sijapenda Fei.

Columnist: www.tanzaniaweb.live