RIPOTI ya CAG imetoa hati yenye mashaka katika ukaguzi wake wa hesabu za serikali kwa Jiji la Dar es Salaam.
Dar ni miongoni mwa taasisi na mashirika ya umma 999 yaliyokaguliwa na CAG kwa ripoti ya 2020-2021 na kuwepo kwenye orodha ya hati 19 zenye mashaka zilizotolewa.
Wengi wanaposikia hati yenye mashaka, wamekuwa hawaelewi mkaguzi anamaanisha nini katika ripoti.
Ufafanuzi wa tafsiri ya hati zinazotolewa na CAG ni huu:
Hati yenye mashaka inatolewa iwapo taarifa za fedha
hazikuonyesha usahihi, kutokukubaliana na uongozi au kukwazwa kwa mawanda ambapo athari yake ni kubwa lakini si muhimu na kwamba ukiacha athari zilizosababisha kutoa hati yenye shaka, taarifa za hesabu zimetengenezwa na kuwepo kutoelewana kwa maelezo ya viongozi husika.
Hati isiyoridhisha inatolewa pale ninapothibitisha kwamba, taarifa za fedha hazikutengenezwa kwa kufuata misingi ya inayokubalika ya utayarishaji wa
taarifa.
Hesabu zilizowasilishwa hazina maelezo ya kutosha ambayo
yanawezesha taarifa za fedha kuelezeka vizuri na kwa upana zaidi.
Hati mbaya au chafu hutolewa wakati uthibitisho wa ukaguzi ni wa
kutosha na hivyo kushindwa kutoa maoni juu ya taarifa za fedha
zilizowasilishwa.
Endapo taarifa za fedha zitakuwa na mapungufu makubwa basi hati chafu hutolewa.
Hati safi hutolewa baada ya ukaguzi kupitia nyaraka na kujilidhisha kuwa kla kitu kiko sawa.