Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

TFF ifanyie kazi madudu ya usajili

B1f4c69874545a67897c270eedcf2f56 TFF ifanyie kazi madudu ya usajili

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANZONI mwa wiki hii, Shirikisho la soka la kimataifa, Fifa liliipiga faini ya karibu sh milioni 300 Simba kwa kukiuka taratibu za usajili.

Simba imekumbana na rungu hilo baada ya kumsajili Shiza Kichuya kutoka Pharco ya Misri bila kuwa na uhamisho wa kimataifa.

Mbali na adhabu hiyo kwa Simba, Kichuya pia aliyewahi kuwika na Simba kabla ya kwenda Misri amefungiwa miezi sita kwa kosa hilo.

Haya ni masikhara, tunasema masikhara kwa sababu taratibu za usajili zinajulikana na Simba ni timu kongwe imeshafanya usajili wa aina hiyo mara nyingi.

Ina maana Simba haikufahamu kama ilipaswa kuwa na uhamisho wa kimataifa kwa mchezaji huyo ndio imsajili na kumtumia?

Kwa upande wa Kichuya nae ina maana hakufahamu kwamba kuondoka kwenye klabu yake bila taarifa na kujiunga na Simba huku akiwa na mkataba alikotoka ni kosa?

Shirikisho la soka Tanzania, TFF, limeruhusu vipi Kichuya acheze Simba akiwa hana uhamisho wa kimataifa? Huu ni mzaha kwenye soka.

Tukitizama tunaona kabisa hapa kuna upindishaji wa taratibu kwenye usajili huu umefanyika ama kwa kukosa umakini ama kwa kukusudia, hii sio sawa.

Taratibu za usajili zinajulikana, na kama haitoshi bado mchezaji huyo kapelekwa Namungo kwa mkopo TFF imeridhia huku akiwa hana uhamisho wa kimataifa.

Mara kadhaa wachezaji walishakwama kuzichezea timu zao kutokana na kukosa vibali, sasa unafanyikaje uzembe kama huo kwa Kichuya, tunaona lipo tatizo mahali kwenye idara za TFF linalopaswa kufanyiwa kazi haraka.

Bado kuna madudu mengi kwenye usajili, na sasa drisha dogo la usajili linafungiliwa Desemba 15, hofu yetu ni kujirudia kwa mambo yaleyale.

Katika usajili huu wa kumalizia msimu, hatutarajii kufanyika madudu kama hayo ama yanayofanana na hayo, hili la Kichuya liendelee kuwa funzo na wahusika wajifunze.

Lakini pia baada ya hatua hii ya Fifa, tunatarajia kuona TFF ikifanya jambo kwa wahusika ili kunyoosha mambo yaende sawa kwenye taasisi hiyo muhimu kwa ustawi wa soka nchini.

Columnist: habarileo.co.tz