Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

TFF, Bodi ya Ligi wanakwama wapi ratiba ya Ligi Kuu?

Ku7r6ey5t.png TFF, Bodi ya Ligi wanakwama wapi ratiba ya Ligi Kuu?

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKATI ratiba ya mechi za Ligi Kuu kwa msimu mpya wa mwaka 2020/2021 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB), lilisema limezingatia kalenda ya matukio yote muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Ratiba hiyo iliyosomwa mbele ya waandishi wa habari na Mtendaji wa TPLB, Almasi Kasongo alisema wamekuja na ratiba ambayo kwa asilimia kubwa itatatua changamoto zilizokuwa zinaleta kizungumkuti kwa misimu kadhaa ya nyuma ikiwemo suala la viporo kwa baadhi ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.

“Kupitia idara yangu tumeandaa ratiba ambayo itakuja kumaliza changamoto zote za msimu uliopita, ikiwemo suala la timu kuwa na viporo vingi kwenye ligi ili kutengeneza usawa na pili imezingatia kalenda ya matukio muhimu ya kitaifa na yale ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la kimataifa, Fifa.

Mashabiki na wadau wa soka walipongeza kwa kuja na mfumo huo ambao kimsingi ilikuja kumaliza kero iliyokuwa inasumbua kwa muda mrefu kwani walikuwa wakiamini ligi hiyo ilikuwa inapoteza mvuto na pengine kupatikana bingwa asiyestahili.

Kabla ya ligi hiyo haijaingia kwenye mzunguko wa tano, TFF kupitia Ofisa Habari wake Cliford Ndimbo walitangaza timu ya Soka ya taifa, Taifa Stars Oktoba 11 dhidi ya Burundi kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Kwa taarifa ambazo zinaendelea kusambaa zinaeleza kwamba huenda mechi hiyo ikavuruga kalenda ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika Oktoba 18 mwaka huu na kusababisha kusogezwa mbele.

Ni wazi sasa mashabiki wanaanza kujiuliza maswali mengi na wakapata majibu kwamba wanarudi kulekule kwenye misimu iliyopita kulalamikia ratiba ya mechi za ligi.

Mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba kama itapelekwa mbele ni wazi bado changamoto ya mechi za viporo kama msimu uliopita itaendelea kusumbua.

Ikumbukwe kwamba hadi sasa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Shirikisho haijaanza kwa maana hiyo itakapoanza maana yake ligi itasimama tena na viporo kuendelea kama kawaida.

Bado wadau wa soka wanaelekeza lawama kwa TFF, kwa kushindwa kutatua changamoto ya upangaji ratiba inakuwaje wasizingatie kalenda za Caf na Fifa wakati michuano ya kimataifa inajulikana.

TFF kupitia Rais wake Wallace Karia wanatakiwa kuisaidia bodi ya ligi kupata wataalamu wa kupanga ratiba itakayozingatia matukio yote ya mwaka.

Kitendo cha kuendelea kujirudia matatizo ya viporo kama misimu iliyopita ni wazi taasisi hiyo inazidi kujitia doa na kuanza kupoteza imani kwa wadau wanaowahubiria kila siku wanapiga.

Columnist: habarileo.co.tz