Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Simba v Ihefu: Mnyama alihitaji akili kubwa

Simba Vs Ihefuuu Kikosi cha Simba kilichoanza vs Ihefu

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kilikuwa ni kitendawili kigumu kukitegua. Ihefu ilijilinda kwa nidhamu ya hali ya juu. Kila mchezaji alishiriki katika kuilinda timu na wakashambulia kwa kushtukiza. Na ndio maana ushindi wa Simba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya mkiani ulikuwa ni ahueni kubwa kwao, yangekuwa matokeo mengine yoyote yangewavuruga sana.

Shabiki yeyote wa Wekundu wa Msimbazi ambaye hakuridhishwa na ubora wa kikosi chake katika mechi mbili zilizotangulia, angebaki na maswali zaidi kama Simba isingeshinda juzi dhidi ya wachovu hao wa ligi kutoka Mbeya.

Licha ya Simba kuibuka na ushindi mwembamba huku wakitawala mchezo huo kwa vipindi vyote walishindwa kuwa na nguvu ya kusukuma mashambulizi makali langoni mwa Ihefu ambao walionekana kujilinda zaidi.

Watu saba wa ukabaji

Ukiondoa kipa wao, Aishi Manula, Simba ilianza na wachezaji saba wa kukaba mabeki wakiwa Shomari Kapombe, Mohamed Husein, Henock Inonga na Onyango viungo wakabaji wakiwa Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Watu hawa wote makocha walilazimika kuwaweka uwanjani wakikosa kiungo mwafaka wa kupandisha mashambulizi na kutengeneza nafasi hasa kutokana na Ihefu kuonyesha kuanzia mwanzo kwamba walikuja na mfumo wa kujilinda zaidi.

Ukiangalia katika kikosi hicho kilichoanza bado hata mabadiliko yanakuja kuingia Nassoro Kapama ambaye pia ni mkabaji na winga mshambuliaji Kibu Denis, utagundua jinsi makocha wa Simba walivyo na wakati mgumu.

Pengo la Chama kubwa

Ukiondoa mechi dhidi ya Mtibwa mshambuliaji Mosses Phiri kupoteza kasi ya kufumania nyavu, katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Singida Big Stars na hii ya Ihefu.

Mbaya zaidi akaanza pamoja na Habib Kyombo ambaye ni rahisi kutabirika kutokuwa na ubora wa kufunga kwa sababu ya kukosa utulivu ambao mshambuliaji anatakiwa kuwa nao.

Kukosekana kwa Chama ambaye mechi dhidi ya Ihefu anafikisha mchezo wa pili akitumikia adhabu yake ya kusimamishwa mechi tatu, kunazidi kuimiza Simba kukosa mtu mbunifu ambaye anaweza kuwarudishia makali washambuliaji hao wa mwisho.

Sakho akili kubwa

Inawezekana kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho akawa na makosa mengi ya ubora lakini juzi akili yake lazima iheshimiwe na Wana Simba kutokana na kuona jinsi walivyokuwa wakihangaika kutafuta bao kama wangeendelea kutaka kuingia zaidi katika eneo la hatari la Ihefu ambao walionekana kufunga njia zote.

Katika dakika ya 62 Ihefu wakiwa wote 11 ndani ya eneo lao la kujilinda walipambana kuwazuia Simba wasipate bao, Sakho akapata akili kubwa ya kujaribu shuti la mbali na kufanikiwa kufunga bao lililoipa pointi hizo tatu muhimu.

Ilikuwa ni vigumu kupata bao kwa kuupenya ukuta ule uliojaa kikosi kizima cha Ihefu, lakini akili ya Sakho ilitegua kitendawili hicho.

Ihefu warudishe kujiamini tu

Ihefu hawana matokeo mazuri, waliwaheshimu Simba kwa kuwa na nidhamu ya ukabaji, hawakutaka kabisa kumiliki mpira lakini hawakuwa na utulivu walipopandisha mashambulizi mbele.

Walimtumia sana mshambuliaji Obrey Chirwa lakini shida yao ikawa kutoongezeka kwa haraka juu wakati walipokuwa wanapanda ili kukamilisha kwa urahisi mashambulizi yao na kujikuta yakiishia kwa mebeki wa kati Inonga na Onyango ambao walikuwa makini sana.

Columnist: Mwanaspoti