Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Simba na kengele ya Uamsho Kutoka kwa Mtani

Sure Boy Kati Kati Katika mechi nne walizokutana msimu huu, Yanga wameshinda mara mbili na kutoa sare mbili

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu mbaya kwa Simba umetamatika rasmi juzi Jumamosi, Tumeshuhudia mechi nne za watani wa jadi,mbaya zaidi Simba hawajashinda mchezo hata mmoja, mbaya kuliko maelezo hawaweka mpira golini kwa Yanga kwenye mechi zote nne ni jambo la kufikirisha.

Lakini hii ni kengele ya kuwaamsha usingizi hawatakiwi kupuuza hata kidogo kuyafanyia kazi mapungufu yao yaliyojitokeza msimu huu, ieleweke mpira ni mchezo wa hadharani hivo kila jambo limeonekana hadharani.

Ushambuliaji

Kama kweli walitamani kumsajili Phiri na Adebayo ila walitamkiwa pesa nyingi wakarudi nyuma, basi wakatoe hizo pesa haraka sana haraka kabisa Simba imeoza mbele wale washambuliaji wake wanazunguka tu hawana quality ya kucheza simba hii tunayoitegemea kutushangaza kufika mbali kimataifa. Watoe pesa wapate huduma nzuri, kama Ahly wanataka kumtoa kwa mkopo Luis kweli wasichelewe wakati ndo huu waboreshe kwanza eneo la ushambuliaji huwezi kuwa na team ya ushindi kama hufungi,washambuliji wa simba ni vibogoyo kwa sasa,hawaumi.

Kuzicheza derby.

Simba waneshindwa kabisa kuicheza derby hata inapotokea wameshinda unawaona kabisa watakaa mda mrefu na kushinda tena tofauti na wenzao Yanga ambao hawana mchezo linalokuja suala la derby nadhani kuna kitu wamekiacha kwa sababu zote hizo lakini hwatakiwi kuacha warejee haraka.

Wajifunze kwa Yanga.

Yanga wamehangaika sana kuipata hii quality ya team waliyonayo sasa, hivyo Simba waisubiri team ife kabisa waanze upya kwa sasa wameteleza tu hawatakiwi kuanguka wabomoe maeneo yote ambayo yameonyesha mapungufu ili msimu ujao kusiwe na 'excuses' nyingi.

Yanga hawajabahatisha kuwafunga Simba msimu huu walijiandaa toka msimu uliopita,kwa sasa Simba waachane na msimu huu waamze kujiandaa na msimu ujao wakati Yanga watakua bado akili zao zipo msimu huu kukamilisha ndoto zao za kutwa vikombe vyote.

Kuanza upya sio ujinga.

Columnist: www.tanzaniaweb.live