Simba wako Morogoro lakini wanaiwaza zaidi mechi ya Horoya AC ya mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Robertinho anajua anaweza kupoteza alama 3 au 2 leo dhidi ya Mtibwa Sugar na isiwe story... Lakini akipoteza dhidi ya Horoya AC anajua ugumu atakaopitia.
Simba wanaweza kupoteza Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili mfululizo, Lakini kama watafuzu hatua ya robo fainali ya CAFCL wanaweza kujipongeza!
Kwa namna timu zetu zilivyo,
Kama Robertinho atashindwa kuchukua Ubingwa msimu huu na akashindwa kuvuka hatua ya makundi basi tujiandae kupokea 'TAARIFA KWA UMMA' inayomhusu! ambayo itazungumza masuala ya kukubaliana kwa pande mbili.
Hivyo Basi, Mchezo wa leo wa Simba Vs Mtibwa Sugar wachezaji na benchi la Ufundi wanaoutazama kwa tahadhari kubwa sana ili usiathiri mechi ijayo.