Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Simba, Yanga namba haziongopi

FtqwmIDWYAAgz G Simba, Yanga namba haziongopi

Sun, 16 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wanasema namba hazidanganyi na ni vigumu kuzibishia hasa katika mchezo wa soka, kwani huwa zinapunguza maelezo marefu ya kufafanua jambo.

Zinaweza zisitoe hitimisho la moja kwa moja la mechi ya soka, lakini zinazisaidia timu kwa maana ya kujua zilikuwa wapi, ziko wapi na muelekeo wake ukoje hasa zinapokuwa na mechi mbele.

Wakati Simba na Yanga zikitarajiwa kukutana katika mechi baina yao, Jumapili hii kuanzia saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, zifuatazo ni baadhi ya dondoo muhimu zinazohusiana na mchezo huo katika namba.

07 Simba haijapata ushindi katika mechi saba mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya Yanga tangu iliposhinda bao 1-0, Februari 16, 2019 ambapo imetoka sare tano na kupoteza mechi mbili.

12 Mabao 12 tu yamefungwa na timu hizo zilipokutana katika mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu ikiwa ni wastani wa bao 1.2 kwa mchezo.

08 Mabao nane kati ya 12 yaliyofungwa katika mechi 10 zilizopita za ligi baina ya Yanga na Simba yamewekwa kimiani na wachezaji wa kigeni huku manne yakifungwa na wazawa.

04 Yanga itahitaji kupata pointi ili itwae rasmi ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ikiwa itaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mechi ya leo Jumapili.

18 Simba inaikabili Yanga ikiwa imetoka kucheza mechi 18 mfululizo za Ligi Kuu bila kupoteza ikipata ushindi mara 14 na kutoka sare nne.

12 Yanga inaivaa Simba ikiwa imepata ushindi katika mechi 12 mfululizo za Ligi Kuu idadi ambayo ndio michezo mfululizo ambayo haijapoteza.

11 Wachezaji kutoka mataifa 10 tofauti wamefunga bao/mabao katika mechi zinazokutanisha Yanga na Simba katika mashindano tofauti. Mataifa hayo ni Tanzania, Zimbabwe, Nigeria, Ghana, Zambia, Uganda, Kenya, Burundi, Brazil, Burkina Faso na DR Congo.

03 Katika vikosi vya sasa, Fiston Mayele ndio mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya mabao katika mechi ya watani wa jadi ambapo amefumania nyavu mara tatu.

110 Pambano la leo litakuwa ni la 110 tangu timu hizo zikutane katika Ligi ya Bara kuanzia 1965.

45 Miaka iliyopita tangu Kariakoo Derby ishuhudie hat trick iliyopigwa na Abdallah Kibadeni 1977.

Columnist: Mwanaspoti