Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Siasa za Kenya zinavyoishangaza Tanzania

SIASA KENYA picha ya pamoja ya viongozi wa Siasa nchini Kenya

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini humo Mjini Mombasa kujadili mwenendo wa Covid19 nchini mwao pia kuhusu umoja na kulinda amani ya taifa hilo katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Viongozi wa vyama vya siasa ambao Rais Kenyatta amekutana nao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Raila Odinga (ODM), Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper), Moses Wetangula (Ford Kenya), and Gideon Moi (KANU) pia Gavana wa Kaunti ya Kakamega na Naibu Kiongozi wa ODM Wycliffe Oparanya nae alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu ya Nairobi Kanze Dane Mararo.

kitendo hicho cha Rais Kenyatta kimeibua "Eti Eti" nyingi mtandaoni kuhusu sintofahamu za kisiasa zinazoendelea nchini.

Ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia, aongee kuhusu mwenendo wa Siasa nchini, kauli iliyowainua viongozi wa vyama vya upinzani nchini, waliojadili kuhusu hali ya kisiasa kwa upande wao.

Masawli mengi yaliyoibuka ni pamoja, uwepo wa kesi nyingi kwa viongozi wa vyama pinzani nchini ambao wamekuwa wakishtumiwa kwa masuala tofauti tofauti uhusiani ya Uhujumu Uchumi.

Wanaharakati wa kisiasa nchi wamejadili kitendo hicho cha ushirikishwaji wa vyama vya upinzani nchini Kenya kama demokrasia halisi ya kisiasa huku wakikosoa mwenendo wa siasa za Tanzania zinazoendelea.

Lakini Rais Samia alitoa kauli ya kuonelea kukutana na vyma Pinzani kwa ajii ya kuzungumza nao, huku upinzani nao wakiwa tayari kukutana na Rais Samia .

Vuguvugu hili la kisiasa bado linakamata kasi hapa nchini, kufuatia kesi ya Ugaidi Mwenyekiti wa CHADEMA, wafuasi wa chama hicho wakisisitiza kiongozi huyo sio Gaidi kama inavyotajwa.

Umoja huu ulioneshwa nchi Kenya miongoni mwa Chama Tawala na Vyama vya Upinzani, umekuwa gumzo kwa kile kinachoendelea sasa nchini, Ikumbukwe kuwa Rais Samia alitoa kauli ya kuonelea kukutana na vyama vya upinzani kwa ajili ya kuzungumza nao, huku Upinzani nao wakionesha utayari wa kukutana na Rais Samia, kinachotazamiwa hapa ni tarehe ya kukutana kwao, ambayo huenda kukutana kwao kukawa mwarobaini wa vuta nikuvute za kisiasa nchini.

Mtazamo wako ni upi kufuatia tambo hizi za kisiasa zinazoendelea , kila pande inatamka haki juu yake, Je danadana hii ya kukutana kwa vyama siasa inatoa taswira gani? je huu ndo ukomavu wa siasa ya Tanzania?

Columnist: www.tanzaniaweb.live