Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Shinyanga mguu kwa mguu katika mapambano kukabili corona

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

•RD, ma-DC waonya mzaha •Asasi mkoa zajiunga kampeni

HALI si nzuri katika kuendeleza mapambano ya kujikinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya corona nchini, uongozi wa kiserikali katika mikoa mbalimbali unaedelea kuchukua hatua za kuelimisha wananchi.

Pia, wadau wa aina mbalimbali, nao wanaendelea na kazi ya utoaji misaada ya vifaa vya kujikinga na maambukizo ya virusi hivyo, ikizingatiwa.

Sehemu ya nyenzo muhimu dhidi ya maambukizo ya virusi vya corona mara mtu anapokuwa katika mkusanyiko wa umma, ni kwamba anawe kwa sabuni na maji tiririka, au kupata huduma za vitakasa, pia kujihami usoni kwa barakoa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, anasema mpaka sasa mkoa wake uko salama, hakuna aliyebainika kuambukizwa virusi vya Covid 19, au watu kukaa karantini na rai yake kwa wakazi ni wajilinde dhidi ya mabumbukizo.

Anaendelea kwa kauli kali: “Kwa wale ambao wanaendekeza mzaha kwenye mapambano ya kujikinga na virusi hivi vya corona, tutawachukulia hatua pamoja na kuwapiga faini.

“Pia, natoa onyo kwa wananchi ambao wanafanya mzaha wa kupiga simu kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, na kudanganya kuwa wana virusi hivyo kumbe hawana tabia hii ife.

“Janga hili ni hatari siyo la kufanyia mzaha, bali kila mmoja achukue tahadhari pamoja na kufuata maelekezo ya serikali ndipo tutabaki salama.”

BOSI SHUWASA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji, Usafi na Mazingira, mjini Shinyanga (Shuwasa), Flaviana Kifizi, katika ziara yake kukagua maeneo mbalimbali ya jamii, kukagua mwitikio wa wananchi dhidi ya tahadhari ya kinga na maambukizo anaeleza kubaini changamoto.

Ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya mkoa kwa matendo, Kifizi anataja kugundua mzaha dhidi ya maagizo, ukiukwaji kanuni na maelekezo sahihi ya kitaifa, ikiwamo ukiukwaji matumizi ya ndoo zisizo zenye vigezo kwa ajili ya kunawa.

Kifizi anaukumbusha umma tahadhari ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona, huku wengine ndoo zikiwa tupu hazina maji ndani.

“Shuwasa tunaungana na serikali kuendeleza mapambano ya kudhibiti maambukizo ya virusi vya Corona,” anasema Kifizi.

VIONGOZI WILAYA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, anakiri kasoro zilizotajwa kuhusu kuwepo mzaha wa kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

Anataja mahali husika, panajumuisha vijiwe vya bodaboda, vilabu vya pombe, baa na kumbi za starehe, ambako kuna mlundikano wa watu na ukosefu wa vifaa vya kunawa na sabuni.

Macha anawakumubsha wananchi wakazo wake kuchukua tahadhari, wakianza na kuweka kando mzaha penye mwingiliano wa umma, hasa kutoka maeneo yaliyoathirika, akitaja mfano wa nchi jirani kama Rwanda, Burundi na Jamhuri wa Kidemokrsia Congo (DRC).

Aidha, jirani yake Jasinta Mboneko, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, anawaagiza maofisa watendaji wa kata na afya, wafanye ukaguzi kuzunguka maeneo ya kijamii yanayoweka ndoo tupu zisizo na maji, ili wahusika wachukuliwe hatua kisheria, kwa kupuuza maelekezo ya serikali.

Mboneko anasema, serikali ilishatoa maelekezo kila penye huduma za kijamii, panapaswa kuwekwa ndoo bora zenye maji ndani yake, ili wananchi wanawe mikono kwa sabuni na majitiririka, kabla ya kupata huduma, ili wajikinge dhidi ya maambukizo ya virusi corona.

“Msaada huu wa ndoo 15 ambazo tumezipokea kutoka kwenye mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Shinyanga (Shuwasa), tutazipeleka zote kwenye maeneo ya Sokoni ili kuongeza nguvu ya wananchi kunawa mikono kwa sabuni na Majitiririka, maeneo ambayo yana msongamano wa watu wengi,” anasema Mboneko na kuongeza:

“Matenki haya mawili ambayo na sisi tumepewa na mgodi huu wa madini ya dhahabu Barrick tuta yapeleka kwenye maeneo ya Standi ya Mabasi, ambapo napo kuna msongamano wa watu wengi, lengo likiwa ni kuongeza nguvu ya kupambana na maambukizo haya ya virusi vya Corona hapa Shinyanga.”

WADAU MIGODI

Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu, Barrick, kupitia mgodi wake wa Buzwagi, wilayani Kahama, umo katika orodha ya wadau wa Shinyanga, wanaoungana na serikali, kuendesha mapambano dhidi ya kudhibiti maambukizo ya virusi vya corona.

Antoinette George, ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama Kazini kwenye mgodi wa, Barrick- Buzwagi, anasema nao wameamua kujiunga na kundi la wadau wa vita dhidi ya Covid 19, kwa kuchangia vifaa vya kujikinga dhidi ya virusi hivyo.

Anataja walivyochangiana idadi yake: Barakoa 400, glovu jozi 50; vipima joto saba; dawa aina ya klorini kilo 45; matenki ya maji 88; na mavazi maalum madaktari wakati wa kutibu wagonjwa wa corona suti 40.

VIONGOZI WILAYA

Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi, anasema ili kuunga juhudi za wadau katika kutoa msaada wao wa vifaa vya kupambana na maambukizo ya virusi vya Corona, atalazimika kuweka askari mgambo katika maeneo ya soko na standi za mabasi, kuwasimamia wananchi kunawa mikono kwa lazima.

Columnist: www.tanzaniaweb.live