Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Samatta maji ya Jioni, Mrithi wake ni nani?

SAMATTAAA Mbwana Samatta

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rekodi zinaonyesha kuwa Mbwana Samatta alizaliwa mwaka 1992, mwakani mwezi wa kumi na mbili anafikisha miaka 30. Ni mchezaji mwenye umuhimu wake akiwa pale mbele kama namba tisa wa Taifa Stars.

Pamoja na sifa hizo zipo baadhi ya mechi huwa anabebeshwa mzigo wa lawama iwapo timu haichezi kwa nguvu ya kutafuta ushindi.

Yale mataifa yenye wigo mpana wa wanasoka wanaocheza Ulaya huwa hayapati tabu kucheza na Stars. Wanamtengea ulinzi maalum wa mabeki wawili na kuyamaliza kabisa makali ya timu yetu.

Niliiona hii hali tulipocheza na Nigeria kule kwao. Ikajirudia tena tulipocheza na Misri hapa kwetu, na kwa mara nyingine ikajirudia kwenye mechi zote tatu tulizocheza za AFCON kule Misri.

Yale magoli yake anayoyafunga akiwa Ulaya ndiyo yanayomuhukumu mpaka anapewa ulinzi wa ziada na mabeki wenye sifa zote kwa maana ya vimo, umakini na nguvu za miili. Ukimkaba vyema Samatta hata Msuva unakuwa umempunguzia makali yake. Kwa bahati mbaya umri hauna urafiki na binadamu yeyote.

Tutakapokuwa kwenye michakato ya kutafuta nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia la mwaka 2026, Samatta atakuwa na miaka 33 na pengine miguu yake haitakuwa na wepesi kama huu wa sasa. Mrithi wake tumeshajiuliza anafanana vipi?

Namtazama Keane kule Uingereza akiwa na msimu mgumu kuelekea Qatar 2022 lakini nina uhakika warithi wake wapo kichwani mwa kocha mkuu Southgate.

Tumeshajiuliza mrithi wa Samatta kama anao uwezo kama alionao yeye? Kama akiliangalia goli mara tatu basi mara mbili atafunga au tunaishia kuwa wepesi wa kumkashifu kila anapokuja kutoka Ulaya akiwa majeruhi!

Makocha wa mataifa kama Senegal, Ghana, Cameroon na mengine makubwa kimpira ya Afrika siku zote wanao wigo mpana wa kuwapata warithi wa nyota wanaotamba katika kipindi fulani.

Watazurura Ulaya kuwafuatilia vijana wanaoibuka huko. Watawatazama vijana wanaoibuka ndani ya ligi kuu kama watawafaa. Pia wanazo timu za vijana za rika mbalimbali kama chanzo kingine cha kuwapa warithi, kwetu sisi tumeshaiandaa kisaikolojia ua tunasubiri muda ufike tuanze kulaumiana?

Columnist: www.tanzaniaweb.live