Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Robertinho Mourinho, nakukumbusha kuhusiana na Phiri - Jembe

Phiri Ntibazonkiza Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hallo Robertinho Mourinho, nakukumbusha kuhusiana na Phiri. Kuna kitu nimekuwa nakifikiria sana lakini naona kimekuwa kikiwagusa wadau wanaouelewa mpira.

Kuhusiana na matumizi ya Saido Ntibazonkiza. Kocha Robertinho anaonekana kumuamini Saido sana ambalo si jambo baya lakini anapaswa kukumbuka mambo mawili muhimu... LEO na KESHO.

LEO Saido yes ana ubora lakini umri wake pia umekwenda. Anaposaidia leo, nani watakuwa msaada wa kesho? Dakika 90 kwake hapana, angalau 60 hadi 75. Hii inamsaisia hata yeye kuwa fresh mechi ijayo.

KESHO Waandaliwe wataotengeneza upana wa kikosi. Mfano Phiri ndiye top scorer wa Simba na huenda aliyumba baada ya kuumia.

Amesharejea na anahitaji muda lakini hawezi kuimarika bila ya kucheza. Lazima Robertinho aanze kumrudisha mchezoni angalau dakika 10...15...20 na kuendelea.

Kuwapa nafasi wachezaji wazuri inawasaidia kuimarika na mchezaji kama Phiri anahitaji nafasi ya kucheza iwe Simba au timu nyingine.

ADVANTAGE Ukiwa na wachezaji kama Saido na Phiri, huhitaji kumchosha mmoja kwa 100%. Phiri ni sharp zaidi inawezekana pia umri wake, ana faida pia ya kupiga miguu yote na anaweza kucheza wingi au inside 10.

Mzoefu na tayari kaonyesha msimu wake wa kwanza Simba na anaongoza kwa mabao katika kikosi hicho. Hivyo Robertinho akubali kumpa muda na siku moja atamsaidia sana.

Maoni haya si lazima leo lakini Robertinho Mourinho akiyafanyia kazi ninaamini yatakuwa na faida kwake hata kama ni baadaye. Ankal Mgunda mfikishie kocha.

Columnist: www.tanzaniaweb.live