Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Pengine Dabi hii tutaona tunachokitaka

Yanga Simba Pic Data Dabi ni zaidi ya matokeo

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Linapokuja suala la 'derby', si kuhusu matokeo tu. Ni kuhusu hisia na kupata heshima kwa hasimu wako wa karibu.

Mara nyingi, matokeo hayahusiani na 'form', hayahusiani na 'class', ni kuhusu kuonyesha shauku na kujali uzito wa tukio.

Rejea tena kilichomtokea Chelsea kwa West ham. Rejea kilichoikuta Barcelona hatari zaidi kwa Espanyol. Miaka mitatu mfululizo hawakuondoka na matokeo pale Estadio Cornella.

Matokeo kama haya yanakuja kwasababu za kawaida za mpira lakini zaidi yanakuja kwasababu ya kusaka heshima na kujali hisia za mashabiki.

Kule America Kusini, ipo derby ya Boca Juniors na River Plate. Mwaka 2006, Bunge liliamua kusitisha shughuli zake kwa wiki moja ili kupisha hii derby. Inaaminika Argentina hakuna kinachozingumzwa zaidi ya hii mechi.

Hapohapo Argentina mwaka 2009, Super Classico ilifika hatua mbaya, hadi mashabiki wa Bocca walifanya jaribio la kuchoma moto jengo la River Plate.

Achilia mbali makumi mechi zao zilizohairishwa kwasababu ya vurugu. Hakuna derby nzito zaidi duniani kuizidi hii ya River Plate na Bocca Juniors. Ni mechi iliyotawaliwa na uhasama unaoambatana na uhuni wa kila namna.

Na hiki ndicho haitakiwi katika soka. Uhuni unaleta madhara kwa wengine kutokana na hisia za derby. Derby itawaliwe na hisia lakini isiambatane na uhuni.

Kuelekea mechi kubwa zaidi nchini, ni vema mashabiki wakatambua derby inahusu sana hisia lakini haipaswi kuambatana na uhuni. Kuharibu rasilimali za nchi kwasababu ya maamuzi mabovu uwanjani ni mfano wa uhuni ninaouzungumzia.

Kikubwa zaidi! Ni mashabiki kuelewa hili soka na kujiandaa kupokea matokeo yoyote. Ni vema kujiaandaa kisaikolojia kupokea kipigo sawa na ambavyo unapokea ushindi.

Haifurahishi kusikia shabiki amepoteza maisha kwasababu timu yake imepoteza mechi. Haifurahishi kusikia shabiki amepata ajali wakati anashangilia ushindi wa timu yake. Nafikiri ni vema kujiandaa kisaikolojia na kujifunza kutawala hisia.

Otherwise! Natamani kushuhudia game nzuri itakayomalizika salama. Tutakutana hapa baada ya mechi.

Columnist: www.tanzaniaweb.live