Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Pamoto! Ni vita ya Phiri, Mbombo Ligi Kuu

Idris Mbombo Pamoto! Ni vita ya Phiri, Mbombo Ligi Kuu

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu Bara inazidi kushika kasi ikiwa katika raundi ya 11, huku nyota wa kigeni wakiendelea kuonyeshana kazi katika kuzibeba timu, lakini vita nzito ikiwa ni kwa mastraika Moses Phiri wa Simba na Idris Mbombo wa Azam.

Nyota hao wameanzisha ligi ndogo baina yao katika kufumania nyavu baada ya wikiendi iliyopita Mbombo kufunga mara mbili wakati Azam ikiizamisha Mtibwa Sugar nyumbani kwao, Manungu, Turiani mkoani Morogoro mabao 4-3.

Juzi pia alifunga bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na bao hilo limemfanya Mbombo kufikisha sita na kumfikia Phiri huku akiipeleka Azam kileleni kwa muda kabla ya kuondolewa na Yanga iliyoshinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na kurejea kileleni.

Wakati ligi hiyo ikiendelea Sixtus Sabilo wa Mbeya City anashika usukani baada ya kuingia kambani mara saba na asisti nne akiwaacha nyuma kwa mabao mawili mastaa hao wa kigeni ambao kwenye Ligi Kuu Bara wapo 28 na wamefunga mabao 57, Mbombo na Phiri ndio vinara kwa upande wao huku jumla ya mabao yaliyofungwa hadi sasa ni 174.

Phiri kwa upande wa Simba amekuwa mchezaji aliyeingia kikosi cha kwanza moja kwa moja kwenye michezo 10 iliyochezwa na ameanza kikosi cha kwanza na kuifungia mabao hayo matano.

Mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa dirisha kubwa la usajili lililopita ameifungia Simba mechi dhidi ya Geita Gold (3-0), Kagera Sugar (2-0), KMC (2-2), Dodoma Jiji (3-0) na Mtibwa Sugar timu yake ikiibuka ya ushindi wa mabao (5-0).

Mbombo sio chaguo la kwanza kikosini katika mechi nyingi wameanzia benchi, huku chache akianza kikosi cha kwanza, lakini ameonyesha umwamba wake wa kuibeba timu ya Azam FC akiwa kinara kutupia mabao matano kambani.

Supastaa huyo wa Azam FC amezifunga Mbeya City timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 1-0, aliifungia timu yake bao la kufutia machozi dhidi ya KMC ikikubali kipigo cha mabao 2-1, dhidi ya Dodoma Jiji aliifungia bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 na ameibeba kwenye ushindi wa mabao 4-3 nyumbani kwa Mtibwa Sugar.

SAKHO vs MAYELE

Vita nyingine kwa nyota wa kigeni ni kati ya Pape Sakho (Simba) na Fiston Mayele (Yanga) ambao tayari wameingia kambani mara tatu na kuzisaidia timu zao kukusanya pointi.

Sakho ameipa pointi Simba dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuifungia bao 1-0 na Pia aliifungia Simba mabao mawili kwenye ushindi wa (5-0) dhidi ya Mtibwa Sugar huku Mayele kafunga mabao matatu kwenye mechi nane walizocheza akikosa moja dhidi ya KMC ambayo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mayele ameifungia Yanga dhidi ya Polisi Tanzania kwenye ushindi wa mabao 2-1, ameifunga Coastal Union kwenye ushindi wa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar pale Yanga walipoibuka na ushindi wa mabao 3-0.

LYANGA, SABILO

Sabilo ambaye ni mchezaji bora wa ligi Oktoba, anaongoza msimamo wa wafungaji akiwa na mabao saba huku Ayub Lyanga wa Azam FC ameingia kwenye vita ya kutoa pasi za mwisho (asists) baada ya Lyanga kufikisha tano na kumuacha nyuma moja Sabilo. Lyanga kinara wa asisti kwa sasa, lakini hajabahatika kutupia bao hata moja na huo ndio utofauti wake na Sabilo.

WENYEWE HAWA HAPA

Akizungumza Mbombo anasema ushindani wenyewe kwa wenyewe utaongeza chachu ya ushindani japo kwa upande wake anafanya hivyo kwa maslahi ya timu na kujitengenezea nafasi nzuri ya kuwa bora.

“Sipo Azam FC kwa ajili ya ushindani na wachezaji walio nje ya timu yangu, japo naamini kama kuna kitu kinafanyika kwa kila mchezaji kuipambania timu kitaongeza chachu ya ubora wa ligi,” anasema mchezaji huyo.

Naye Phiri anasema anaangalia nini kilicho mbele yake, lakini haangalii nani anamkimbiza lengo likiwa ni timu yake kupata matokeo mazuri ili iendelee kupambania kutwaa taji msimu. “Kila mmoja aipambanie timu yake tukutane mwiosho wa msimu suala la kujua nani kafikia mabao ya fulani sio muhimu sana kwangu naangalia ni namna gani niisaidie timu yangu ipate matokeo,” anasema.

Columnist: Mwanaspoti