Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Paa wa Bahamas Mwanamke hodari wa riadha ya Omlipiki

Olympic Pic Paa wa Bahamas Mwanamke hodari wa riadha ya Omlipiki

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Katika miaka 227 ya mashindano ya Olimpiki wana michezo 850 (wanaume 590 na wanawake 260) wameshiriki mashindano haya mara tano, yaani kwa kipindi cha miaka 20.

Katika mashindano haya ya michezo mbalimbali ya wanaume, wanawake inayofanyika baada ya miaka minne wanaodumu kwa muda mrefu ni washiriki wa michezo isiohitaji sulubu.

Anayefanikia kuwepo kwa muda mrefu katika kandanda, riadha, ndondi au kuogelea huwa amefanya jambo lisio la kawaida na miongoni mwa wachache waliofanya hivyo ni Pauline Elaine Johnson wa visiwa vya Bahamas.

Katika kuukaribisha mwaka 2023 miongoni mwa wana michezo waliopata tunzo nyingi kwao, nchi jirani na kutoka kwa mfalme wa Uingereza, Charles Philip ni Pauline.

Alipokuwa kijana (sasa ana miaka 57) aliwika katika riadha na kuwa nyota katika mbio za masafa mafupi. Aliitwa 'Paa wa Bahama' na wengine walimuita ‘Mwanamke wa Dhahabu' wa Carribean.

Katika michezo ya Olimpiki ya Sydney ya 2000 alishinda medali ya fedha na ya shaba na kubeba medali nyingi za mbio za mita 100, 200 na 400 katika mashindano ya kimataifa.

Alipenda kukimbia tokea mdogo, lakini alikataa kushiriki mashindano na ilibidi alazimishwe kufanya hivyo na mjomba wake, Philip Davis, ambaye sasa ni Waziri Mkuu wa Bahamas.

Pauline pia alicheza mpira wa magongo na mara nyingi alilivunja gongo kwa hasira alipokosa kufunga bao la wazi.

Akiwa na miaka 13 kocha Neville Wisdom wa klabu ya riadha alipokuwa anaangalia mkanda wa video alimuona Pauline kuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika mbio za masafa mafupi, lakini hakuwa akijituma vya kutosha.

Wisdom alimtafuta Pauline ambaye hajawahi kumtia machoni licha ya Bahamas kuwa kisiwa kidogo chenye urefu wa maili 21 na upana wa maili 7.

Wakati huo alikuwa akisoma shule ya sekondari, lakini alipokutana naye alikataa kuzungumza kwa vile baba yake, Lincoln, alimkataza asizungumze na wanaume asiowajua.

Hata hivyo, alifanikiwa baba yake alikubali kuonana na Wisdom, lakini alipokwenda nyumbani kwake alikuwa hajarudi kazini. Pauline ndiye aliyemfungulia mlango na kumtaka abaki nje kama mlinzi hadi mzee arudi.

“Huna haki ya kuingia ndani kama baba hayupo”, alimwambia. Mzee Lincoln alipofika, Wisdom alimueleza kuwa binti yake ana kipaji cha kukimbia mbio za masafa mafupi na kumtaka ajiunge na klabu yake ya riadha ya Bain.

Pauline alikataa kwa sababu hakutaka kuwa mbali na baba yake na kusema alikimbia ili kujifurahisha na sio kushindana na kwahivyo hakuhitaji mafunzo.

Baada ya baba yake kumtaka ajaribu na atabaki nyumbani Pauline alikubali shingo upande.

Siku ya pili alfajiri, Wisdom alifika nyumbani kumuamsha kwa kugonga dirisha la chumba chake.

Pauline hakujibu na kocha aliondoka na kuendelea kumgongea kila alfajiri kwa wiki mbili hadi siku moja alitoka nje na kukiri alikuwa akiamka, lakini utamu wa usingizi wa alfajiri ulimfanya abane kimya.

Alipoingia garini alikutana na wasichana wawili, mmoja alimfahamu. Huo ukawa mwanzo wa mazoezi yaliompatia mafanikio.

Pauline anasema mara nyingi kuwa alikataa kufuata maelekezo aliyopewa kwa matumaini angefukuzwa, lakini baadaye aliamua kumsikiliza kocha alipoona hakuwa na njia ya kupenya.

Bibi huyu alifahamika Bahamas kama mkimbiaji mzuri na alishiriki kwa mara ya kwanza 1984 mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Los Angeles, Marekani. Pauline alipewa heshima ya kushika bendera ya Bahamas katika gwaride la ufunguzi.

Katika mbio za mita 100 alitolewa nusu fainali na wataalamu walisema alikuwa bado haonyeshi juhudi na angefanya asingekosa angalau medali ya shaba.

Katika heka heka za Olimpki huko Korea ya Kusini 1988 na ya tatu 1992 , Pauline alifika nusu fainali kwenye mita 100 na 200.

Alikuwemo kikosi cha Bahamas kilichochokua medali za dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti akiwa pamoja na Sevatheda Fynes, Chandra Sturrup, Debbie Ferguson na rafiki yake mkubwa, Eldece Clarke-Lewis.

Pauline akiwa mkimbiaji wa mwisho alipokea kijiti akiwa wa nne, lakini alithibitisha kuwa 'Paa wa Bahamas' kwa kuwapita wakimbiaji watatu waliokuwa mbele, mmoja baada ya mwingine na wa mwisho mita moja kabla ya kufikia utepe.

Huku akishiriki mashindano Pauline hakuwa na mzaha katika masomo na alipopata shahada ya kwanza ya mawasiliano alikwenda Ufaransa.Alipofika New York alikuta ndege ya kwenda Ufaransa imeondoka na imambidi alilala kwenye mabao ya uwanjani.

Aliondoka siku ya pili na alipofika Ufaransa ambayo wakati ule ilikumbwa na miripuko ya mabomu ya magaidi ilimkumba balaa kwa vile hapakuwepo habari za kufika kwake na akakosa mtu wa kumpokea.

Kwa kuwa hajuwi Kifaransa alipata shida kujieleza na ilibidi ahangaike na mkoba wake wa nguo aliuacha ktoa taarifa. Alipokwenda kupiga simu kibandani palitokea mripuko.

Alipoukimbilia mkoba wake kuokoa nguo zake askari polisi wawili walimvamia na kumbeba juu kwa juu huku akilia.

Alipelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashitaka ya ugaidi. Alipoona haelewani na askari alikaa kimya na ilichukua masaa polisi wakiupekua na kuona viatu vya mwana riadha.

Baada ya kuangalia hati yake ya safari na kutambua waliyemtia mbaroni ni Paa wa Bahamas walisikitika na kumuachia kwenda kushiriki mashindano.

Pauline alikwenda hoteli na aliondoka baada ya muda mfupi kwenda uwanjani ambapo alifika dakika chache kabla ya mbio za mita 200 kuanza. Alikimbia kwa kutumia sekunde 22.66 na kutokea wa pili.

Mwaka uliofuata alikimbiwa na ndege alipokuwa Italia na ilibidi alale uwanjani. Usingizi ulipomchukua aliamshwa na askari polisi aliyemuelekezea mtutu wa bunduki.

“Nilishituka na mkojo ulinitoka,” alieleza.

Alikaa mahabusu kwa nusu saa akibishana na askari wenye silaha ambao hakuelewana kutokana na matataizo ya lugha.

Askari mmoja aliposikia zogo alikwenda kujuwa kilichotokea na alipomuona Pauline aliwaambia wenzake; "Huyu ndiye Paa wa Bahamas niliyemuona akikimbia juzi”.

Aliachiwa na kutafutiwa ndege ya kurudi Bahamas.

Alistaafu mwaka 2000 akiwa na miaka 34 baada ya kushiriki mashindano kwa miaka 20 na alitunukiwa tunzo ya OBE ya Jumuiya ya Madola na Malkia Elizabeth wa Uingereza mwaka 2004.

Miaka miwili kabla ya kustaafu alifunga ndoa na mrukaji viunzi wa Jamaica, Mark Thompson, aliyekutana naye katika michezo ya Olimpiki ya 1992 iliyofanyika Barcelona.

Hadi hivi karibuni alikuwa mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Kimataifa la Wanariadha Wanawake .

Columnist: Mwanaspoti