Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Opah Clement yale mabao yake yasubiriwa Besiktas

A27B9240 8A06 427F 8794 BCB6345C0772.jpeg Opah Clement yale mabao yake yasubiriwa Besiktas

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Siku chache zilizopita uongozi wa klabu ya Simba ulifikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa Simba Queens, Opah Clement kwenda kwa miamba ya soka la Uturuki, Besiktas ambako ameanza maisha yake mapya huku kocha wa kikosi hicho, Mesut Kir akiwa na matumaini makubwa kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Kitanzania.

Opah ambaye aliondoka nchini akiwa kinara wa mabao kwenye Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza akiwa na mabao tisa, anatazamiwa kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kwenye kikosi hicho kwa siku chache za usoni kwa mujibu wa Mesut ambaye amekuwa akivutiwa naye.

Nguvu ya ushindani ya kikosi cha Besiktas kwa upande wa Wanawake inaonekana kupungua hivyo kutua kwa nyota huyo ni moja kati ya maboresho ambayo yanatazamiwa huenda yakawa na tija, wababe hao wamemaliza ngazi ya kwanza ya ligi yao wakiwa nafasi ya nne kati ya timu tisa za kundi A, wanakibarua cha kuanzia raundi ya kwanza kupigania nafasi ya kwenda robo fainali kwani ligi hiyo ni tofauti kidogo kimuundo.

Ligi yao ikoje? Wanacheza kwenye mfumo wa makundi ambayo yapo mawili moja likuwa A na timu tisa huku lingine B likuwa na timu 10, wababe wawili kwenye kila kundi wanatinga hatua ya robo fainali huku timu nyingine kulingana na nafasi walizopo kwenye makundi yote mawili hucheza raundi ya kwanza ambapo huchuana ili kupata wababe sita.

Wababe hao sita hukumbana na wale ambao walimaliza vinara kwenye makundi hayo hivyo jumla kuwa timu nane ambazo zitacheza hatua hiyo ya robo kisha nusu na timu mbili zitatinga fainali kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Uturuki.

Akiongea na Nje ya Bongo, kocha mpya wa Opah, Mesut anasema hawatampa presha mshambuliaji wao huyo na badala yake atajengwa taratibu kabla ya kuanza kupewa jukumu la kuongoza mashambulizi ya timu hiyo inayosaka ubingwa ligi ili kupata nafasi ya msimu ujao kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya upande wa Wanawake.

"Anaweza kuwa kipenzi cha mashabiki wa Besiktas, ni binti mdogo ambaye ana nafasi ya kukua na kufanya makubwa zaidi, ana kipaji kikubwa ambacho naamini kitaongeza changamoto ya namba kwenye kikosi chetu, sidhani kama anaweza kukumbana na changamoto ya kuendana na mpira wetu kwa sababu hii sio mara yake ya kwanza kuwa Uturuki."

"Kikubwa ni kujua utamaduni wetu wa uchezaji na kuzoeana na wachezaji wenzake baada ya hapo kila kitu kitakuwa sawa mbele ya safari," anasema kocha huyo.

Kwa upande wa Opah nafasi ya kujiunga na miamba hiyo ya soka la Uturuki ni jambo kubwa na kilichobaki ni kuonyesha thamani yake uwanjani, "Natazama mbele, kufanya kile ambacho kitawezekana ili kufikia malengo yangu binafsi na timu."

Katika raundi ya kwanza ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku chache zijazo baada ya michezo ya makundi kumalizika, chama la Opah litaanzia ugenini kucheza dhidi ya 1207 Antalya Spor ambayo kwenye kundi B ilishika nafasi ya tano ikiwa na pointi 25 kwenye michezo 18. Besiktas ilikusanya pointi 24 kwenye michezo 16.

LIGI YA MABINGWA

Besiktas imeshiriki mara mbili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya upande wa Wanawake, msimu wao wa kwanza ni 2019/20 na waliishia katika hatua ya makundi baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi namba tisa nyuma ya Twente.

Mabingwa hao wa zamani wa Uturuki walimaliza hatua hiyo wakiwa na pointi sita walzidiwa na Twente ya Uholanzi kwa pointi mbili ni timu moja tu ambayo ilikuwa ikisonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo Lyon ya Ufaransa ilitwaa ubingwa. Msimu wao wa mwisho kushiriki ilikuwa uliopita, nao hawakufua dafu.

Columnist: Mwanaspoti