Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ni elimu ya amali au ufundi?

Ufundi Amali Emlimu.png Ni elimu ya amali au ufundi?

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kuna maneno yanayosikika sana kwa sasa katika sekta ya elimu ni; elimu ya amali.

Tangu Rais Samia Suluhu Hassan achokoze mjadala wa kitaifa kwa kuagiza kufanyike mapinduzi ya mfumo wa elimu nchini na hatimaye watendaji wake kuingia kazini na kufanya maboresho ya mtalaa wa elimu ya msingi na sekondari, maneno elimu ya amali yameshika chati. Ni sawa na kusema ndio gumzo kwa sasa katika duru za kielimu na hata kwenye vilinge vya wadau wa elimu.

Waziri Mkenda na elimu ya amali

Oktoba 10 mwaka 2023, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, aligusia kwa nini Serikali imeanzisha elimu ya amali nchini.

Alisema lengo la Serikali ni kutaka kutoa elimu bora kwa wanafunzi ambapo watakapomaliza wawe na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa, hivyo sekta binafsi kama wadau wajitokeze kwa ajili ya kutimiza lengo hilo la Serikali.

“Kwenye elimu hii ya amali tutakuwa na michezo, kilimo pamoja na ufundi ambapo mtoto atakapomaliza kusoma atapata na cheti chake alichosomea hivyo nawaomba kama kuna mtu ana uwezo wa kutoa elimu hii awasiliane na Serikali na sisi tutaboresha mazingira yake,” alisema Profesa Mkenda alipokuwa akizipigia chaapuo shule binafsi kujikita kuomba fursa ya kufundisha elimu hiyo.

Upo mgongano?

Lakini unajua kama elimu ya amali inawakanganya baadhi ya watu? Swali ni hili: je, elimu ya amali ambayo ni maarufu katika visiwa vya karafuu inatofautiana vipi na elimu ya ufundi?

Swali jingine ni hili; kulikuwa na haja gani ya kuja na ‘ubunifu’ wa elimu ya amali, wakati tayari tulishakuwa na elimu ya ufundi tena ufundi stadi katika vyuo vya Veta?

Kujua kama elimu ya amali ndio elimu ya ufundi au vinginevyo, Mwananchi tunachofanya ni kunukuu hapa baadhi ya fani zinazopendekezwa kwenye mtalaa wa elimu ya amali kama tulivyoyatoa katika nyaraka za Serikali,

Sasa kibarua kitakuwa kwako, kuita masomo hayo ni elimu ya amali au elimu ya ufundi? Tuone baadhi ya masomo hayo:

Electrical installation, Mechanical Engineering, Civil Engineering, Automotive Engineering, Transport and logistics, Clothing and Textile, Agriculture and Food

Processing

Fani nyingine ni Hospitality and Tourism, Commercial and Business, Support Service, printing, extraction and processing of minerals, cosmetology, creative arts, ICT and electronics na Sports.

Columnist: www.tanzaniaweb.live