Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nenda Mzee Mkapa ila kwa hili umetuheshimisha na hatutokusahau

WhatsApp Image 2020 07 24 At 09.49.54.jpeg?fit=720%2C415 Nenda Mzee Mkapa ila kwa hili umetuheshimisha na hatutokusahau

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: dar24.com

Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amelitangazia taifa usiku wa kuamkia leo kifo cha aliyekuwa raisi wa Tanzania mzee wetu Benjamin William Mkapa.

Hakika hii ni huzuni kwa kila Mtanzania na mzalendo lakini kwa sisi watu wa soka mzee Mkapa atadumu mioyoni mwetu kila tukiutazama urithi alitouachia wa UWANJA WA TAIFA WA KISASA.

Wazo la uwanja huu wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000 lilikuja katika awamu yake na mwaka 2005 uwanja huu ulianza kutengenezwa na kufunguliwa 2007 ikiwa moja ya viwanja bora sana barani Afrika.

PUMZIKA KWA AMANI (RIP) BENJAMIN WILLIAM MKAPA, NA ASANTE KWA ULIYOTUFANYIA.

Columnist: dar24.com