Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nchi zinazodaiwa michango EAC zilipe kufikia malengo

EAC Nchi zinazodaiwa michango EAC zilipe kufikia malengo

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIKA siku za karibuni, kumekuwa na taarifa za changamoto mbalimbali zinazokabili Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Bunge la jumuiya hiyo kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake kutokana na baadhi ya nchi kushindwa kulipa tozo za mwaka.

Michango ya nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki ndizo zinazowezesha Sekretarieti ya EAC kupanga mipango yake, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa hatua mbalimbali za mtangamano wa jumuiya kwa lengo la kuwawezesha wananchi wa jumuiya kuungana katika nyanja za kibiashara na mengineyo.

Ni dhahiri kuwa kutokana na uendeshaji wa shughuli za jumuiya unatokana na michango, hivyo kila nchi ina wajibu wa kuhakikisha katika mipango ya maendeleo inaipa kipaumbele michango hiyo kwa maendeleo ya jumuiya.

Inaelezwa kuwa kati ya masuala muhimu yaliyokwama kutokana na baadhi ya nchi kutotoa michango kwa wakati mpango kazi wa miaka 10 itifaki ya umoja wa fedha iliyosainiwa mwaka 2013 na kupitishwa na nchi zote ambapo mwaka 2018 Bunge la EALA ilipitisha kuundwa kwa taasisi ya fedha ya Afrika Mashariki na ile ya takwimu na sheria ya kuundwa vyama hivyo kupewa ridhaa na wakuu wa nchi.

Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Dk Abdullah Makame anaeleza kuwa kutokana na changamoto ya fedha, taasisi hizo zimebaki katika makaratasi na ujenzi wake haujaanza hivyo kuwa changamoto kufikia malengo, ikiwemo wananchi wa EAC kupata ajira kwenye taasisi hizo.

Inaelezwa kuwa katika nchi hizo sita za EAC, Kenya ndiyo nchi pekee isiyodaiwa huku Tanzania ikiwa imelipa bajeti kuu kwenye sekretarieti imeishalipa zote na dola milioni 4.2 zinazodaiwa ni deni la baraza ya vyuo vikuu vya Afrika mashariki Tanzania kwa miaka miwili pamoja na michango katika taasisi ya uvuvi ya ziwa Victoria Awali, Mbunge wa EALA kutoka Kenya, Abdikadir Aden alilieleza kuwa wabunge wa EALA wamekuwa wakipokea mishahara ya dola 6,408 pamoja na posho ya dola 14,000 huku wakilipwa dola 160 kwa kila kikao, ikiwemo ambao nchi zao hawajalipa michango.

Alisema kila nchi mwanachama inatakiwa kulipa dola milioni nane kila mwaka kama mchango kwa nchi hiyo, lakini mpaka Juni 10 mwaka huu Burundi iliyojiunga na EAC mwaka 2007 ina malimbikizo ya miaka miwili na kudaiwa dola milioni 15.

Huku Sudan Kusini ikidaiwa dola milioni 27 baada ya kujiunga mwaka 2016 ikiwa nchi ya sita kuwa mwanachama. Kutokana na madeni hayo kwa kila nchi ni ngumu kwa Sekretarieti ya EAC na bunge kutekeleza majukumu yake inavyostahili, hivyo ni vema nchi hizo kila mmoja kuona umuhimu wa kuhakikisha kila mwaka inalipa madeni ili bila kulimbikiza kuwezesha malengo ya jumuiya yanatekelezwa.

Katika kuhakikisha kuwa ushirikiano katika jumuiya ni wa kindugu ndiyo sababu ya kuwa huduma zote zinatolewa kwa usawa hata kwa wabunge na wafanyakazi kutoka nchi ambazo hazijalipa michango kuendelewa kupewa huduma zote, ikiwemo mishahara na posho.

Kutokana na upendo huo, si vema kusubiri mpaka kupewa vitisho vya kusitishiwa uanachama au kujadiliana kwenye vikao vya jumuiya na kuacha kujadili masuala ya maendeleo. Ni vema kila nchi ilipe na viongozi wa nchi wahakikishiwe katika bajeti zao suala la michango kwenye EAC na jumuiya nyingine za kimataifa zinapewa kipaumbele.

Columnist: habarileo.co.tz