Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nchi za EAC zitekeleze itifaki kwa pamoja

114c890cb9c174af950e33ccddca6195 Nchi za EAC zitekeleze itifaki kwa pamoja

Tue, 4 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MOJA ya shabaha ya kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni utekelezwaji wa Itifaki ya Forodha ambapo nchi zote zinafanya biashara ya pamoja ikilenga kujenga miundombinu ya kuvutia uwekezaji wa kimataifa.

Itifaki nyingine ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kusimama kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na Itifaki ya Soko la Pamoja, Itifaki ya Sarafu Moja ambayo mchakato wake unaendelea na Shirikisho la nchi moja.

Utekelezwaji wa itifaki zote hizi unategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa karibu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kuepusha tofauti ambazo zinaweza kujitokeza katika utekelezaji wake.

Itifaki ya Forodha na Soko la pamoja ndio msingi wa wazo langu kutokana na ubabaishaji ambao umekuwa ukijitokeza miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ndio wadau wakubwa wa jumuiya hiyo.

Huu ndio msingi wa kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya sheria namba 75 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kupitia itifaki hiyo nchi zote za Afrika Mashariki ziko huru kufanya biashara katika nchi nyingine.

Nchi zote zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki zinapaswa kutekeleza kipengele hiki ili kuondoa misuguano isiyokuwa ya lazima.

Nchi zote zilikubali zitasaini kuwa zitatekeleza kwa moyo mkunjufu, sasa kwa nini kunakuwa na ubabaishaji? Kupitia mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania ina haki ya kufanya biashara nchini Uganda, Burundi, Sudan Kusini, Kenya na Rwanda.

Hali kadhalika nchi nyingine zote zina haki ya kufanya biashara na Tanzania bila kuzuiwa kulingana na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Janga la virusi vya corona ndilo lililopunguza ushirikiano baina ya nchi za Afrika Mashariki.

Baada ya nchi zote kufungua biashara, ni mategemeo yetu kila nchi ifungue milango ya biashara kwa nchi nyingine ili kuhakikisha kuwa mkataba huo unatendewa haki.

Katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo ya kwanza kufungua milango ya biashara na mataifa ya nje kutokana na kushuka kwa idadi ya wagonjwa wa covid- 19.

Nchi zote za Afrika Mashariki zilikaribishwa kufanya biashara zao Tanzania. Bahati nzuri ni kuwa kuanzia Agosti Mosi, 2020 mataifa mengine ya Afrika Mashariki yalifungua anga na biashara zake na nchi za nje.

Baadhi ya mataifa hayo ni pamoja na Kenya, Rwanda na Sudan Kusini. Baadhi ya nchi kutoka Afrika Mashariki ziliwekewa vikwazo vya kushiriki biashara kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi makubwa ya virusi vya corona miongoni mwa nchi wanachaama na kusababisha taharuki kubwa ambayo mwisho wa siku zililazimika kutafuta maridhiano ya kibiashara.

Baadhi ya wachambuzi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki walielezea kitendo hicho kuwa ni mbinu za kibiashara za kuweza kushinda soko la kiushindani hasa miongoni mwa nchi shindani kibiashara.

Ili kumaliza mivutano isiyokuwa na msaada kwa uchumi wa Afrika Mashariki, wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia walishauri nchi hizo kurejea katika itifaki zilizounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Columnist: habarileo.co.tz