Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Nasaha za wakuu wa nchi kwa watendaji wake

BARAZA Nasaha za wakuu wa nchi kwa watendaji wake

Fri, 8 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

• Walakini kukabili corona ‘unatumbua’ uchumi

KINACHOTOKEA sasa kiko katika kumbukumbu za zama zinazohusika na mashairi ya ugonjwa corona, kutoka kila kona.

Kama ulivyo mfumo na maisha ya kibinadamu, jambo moja huzua mabadiliko katika lingine. Inapokuwa katika sura ya uchumi inabeba jina ‘multiplier effect’ ambayo ina tafsiri kubwa.

Maana inayobebwa jambo moja linazaa mengine. Mfano ni pale mwanafamilia akipata ajira, nyendo za mlo na kujiendeleza kwa wanafamilia unapanuka.

Inapofuatilia kwa kina mkasa wa corona nchini walau katika eneo dogo kuweka mantiki ndani ya walau maeneo mawili, moja kutoka kauli ya Rais Dk. John Magufuli akiwa nyumbani Chato na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, tayari kuna tafsiri kubwa, kiuchumi na kibiashara kitaifa.

Hapo ndipo kabla ya kupiga hatua zaidi kunapaswa kuzama katika maana zake za ujumla, kwamba uchumi unasimamia mantiki namna rasilimali kidogo zinavyoweza kukidhi mahitaji muhimu kwa kiwango cha juu kadri inavyowezekana.

Vivyo hivyo, biashara inabeba tafsiri ya shughuli za kubadilishana bidhaa au huduma kwa kiwango maalum cha mabadilishano ambayo ndio bei tajwa.

Ubora wa uchumi ni namna matumizi ya rasilimali yanavyokidhi kiwango cha juu cha matakwa sahihi ya jamii au mtu husika. Hapo biashara inapaswa kufanyika katika mfumo wa haki sawa kuwezesha malengo.

Huo ndio mzizi wa kuanzishwa Tume ya Ushindani Sawa katika Biashara nchini. Mchakato kuanzia taratibu za ununuzi hadi upande wa pili wa mauzo na taratibu zote za malipo, zinapaswa kuwa sahihi kitaaluma na kisheria. Kuna bodi inayohusika kusimamia ununuzi na nyingine ukaguzi wa hesabu ya umma (CAG).

Katika zama zilizopo za vita dhidi ya ugonjwa corona, Je, hizo zinafuatwa? Hapo inaanzia tafsIri ya uchumi kutumia vyema rasilimali za umma kukabili janga hilo linaloshambulia rasilimali muhimu katika uchumi, kwa maana ya watu.

Pia, kutetea makusanyo yatokanayo na kodi zao na kuwaweka huru kisaikolijia ili wazalishe.

Biashara nayo inafanyika katika mfumo na taratibu sahihi kitaaluma na kisheria, ili mwenendo wa kiuchumi uende katika mustakabali stahiki, mathlan kudhibiti mfumuko wa bei kutoka kwenye bidhaa za viwandani na vyakula?

Mapengo yanayojitokeza sasa nchini, alianza nayo kuainisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni katika Ibada ya kitaifa jijini Dar es Salaam, alipoweka wazi hakuna uhaba wa sukari kitaifa na hata kiasi kidogo ambacho ni pengo kitaifa kilishaagizwa.

Hiyo ilitokana na kilichomshangaza ndani ya wiki kadhaa nchini bei ya sukari rejareja kuruka kutoka wastani wa Sh. 2,500 kwa kila hadi Sh. 4,000 na wananchi kuhangaika mno hadi sasa, huku katika ngazi ya juu si picha nzuri, kunakaribisha hali ngumu na mfumuko wa bei kwa wananchi.

Tayari kuna hatua zimeshachukuliwa kufuatilia hayo ya ubabaishaji katika biashara ya sukari, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kufuatilia sokoni ‘mguu kwa mguu’ na wanaopotosha bei kwa kurundika ghalani mzigo wachukuliwe hatua.

Ni tendo ambalo si mara ya kwanza kutokea na hata serikali ikachukua hatua inayostahili, dhidi ya wafanyabiashara.

Kurejea kwa Rais Dk. Magufuli, msomi wa kemia na hisabati za darasani, alionyesha kukerwa na baadhi ya hatua dhidi ya kukabili corona, zikiwa na athari za kiuchumi na kibiashara.

Anataja mbinu za kudhibiti ueneaji corona ikiwamo jijini Dar es Salaam, kwa kunyunyizia dawa mitaani, ambazo hakukubaliana nazo.

Katika ufafanuzi wake kitaalamu ulioendana na kauli ya kukemea, anasema haiendani kabisa na vita sahihi. Hapo inazaa maswali kutaka kuelewa mantiki ya ununuzi sahihi wa huduma hiyo imetokea wapi?.

Katika taaluma na miongozo ya kisheria, ili ununuzi kufanyika, unapaswa kuwa na vitu vitano au inavyoeleweka katika taaluma hiyo ‘5 R’ (Five Rights), kwa maana ya: Idadi kamili, ubora, chanzo, bei na muda sahihi.

Kwa kurejea kilichotamkwa na Rais Dk. Magufuli, kunazaa swali je, wahusika walifuata kanuni sahihi za ununuzi? Kwa maana kila ununuzi wa ofisi ya umma, una mtaaluma anayetumikia?.

Pili, kwa mustakabali huo wa swali la Rais, inazua maswali hata katika matukio wa kanuni za fedha hadi kuidhinishwa malipo ya dawa hizo.

Kama ndani ya vita vilivyopo kukabili ugonjwa corona inafuatwa tafsiri ya uchumi ‘namna bora ya kutumia rasilimali kidogo kwa manufaa makubwa kukidhi maslahi ya umma au watu” inaacha kitendawili kulikonI hatua hiyo kufikiwa?

Pia, kuna eneo ambalo Rais Dk. Magufuli amehoji umma kutishwa kwa kiwango cha juu kuhusu corona, ambayo haina tafsiri nzuri kwa ari na wajibu wao kujitokeza katika uzalishaji mali kitaifa.

Kwa mjumuisho, walakini katika kukabili corona, ina ishara mbaya kwa uchumi kitaifa.

Columnist: www.tanzaniaweb.live