Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Namna ulivyo unene kupindukia na madhara yake yanavyokuwa

UNENE.jfif Namna ulivyo unene kupindukia na madhara yake yanavyokuwa

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), kupitia miongozo yake inaitahadharisha jamii kuhusu kuwapo ongezeko la watu wenye unene wa kupitiliza, ikitaja sababu ya kuwapo watu wengi wenye maradhi ya moyo, kisukari na ini.

Kamusi ya Kiswahili Sanifu, inautafsiri unene ni hali ya mtu kujaa au kutuna mwili. Utafiti duniani, unaonyesha kwamba tatizo la unene uliopitiliza duniani huwakumba wanaume zaidi kuliko wanawake.

Mara nyingi unasababishwa na kawaida ya mtu kula chakula kingi na mwili husika unakosa mazoezi ya kutosha.

Pia, kuna visababishi mwilini pale unapokosa mazoezi yanayostahili unene unaongezeka pasipo vikwazo vya kikomo.

Urithi wa asili wa vinasaba katika familia au ukoo ambao huko nyuma ulikuwa na watu wenye maumbile hayo ya unene.

Kuna suasa la matumizi ya dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa huzaa athari, vyote vinachangia shida ya kuongezeka uzito wa mwili.

Utafiti unaonyesha kwamba watu wanene wanaathirika zaidi na maradhi hayo, kuliko wenzao wembamba.

UNAJIPIMAJE UZITO?

Kupima uzito kwa jina la kitaalamu kunaitwa ‘Body Mass Index au kwa kifupi BMI. Msingi wake, ni kipimo kinachotumia urefu na uzito wa mtu, kujua usahihi alikosimama kiafya, kwa kupata uwiano wake ( uzani wa mita na kilo).

Kwa mujibu wa WHO, inapotokea chini ya wastani 18.5, maana yake ni kwamba, kuna uzito mdogo; na ikiwa kati ya 18.5 na 24.9 unaakuwa uzito wa kawada kiafya ; kati ya 25 na 29.9 unakuwa uzito mkubwa; ilhali zaidi ya 30 unakuwa uzito mkubwa kupindukia.

MADHARA

Kuwa mzito mno kunaleta hatari nyingi kwa afya na kusababisha matatizo au kuongeza uwezekano wa magonjwa mengi sana.

Athari ya kwanza, ni waathirika kushuhudia ongezeko magonjwa kama vile shinikizo la damu, kisukari figo, moyo.

Unene pia unawaletea kinababa tezi dume na kinamama, wapo wanaokumbwa na tatizo uvimbe tumboni.

Pia, kwa hao wenye uzito mkubwa hupungukiwa uwezo wako wa kufikiria (IQ), baadhi wanabaki katika kiwango waalichokuwa nacho miaka 10 iliyopita.

Mnene anaelemewa na shida ya kupumua, ikiendana na matatizo ya kukoroma sana anapokuwa usingizini.

Katika orodha ndefu ya matatizo, kuna suala la mwili kuongezeka mafuta mengi na wakati huohuo, unachoka haraka.

Yapo madhara ya wanene kuwa na kawaida ya kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na maumivu makali kwenye viungo, kama vile magoti na kiuno.

Mifumo yao ya kumeng’enyua chakula, nayo hukaaa vibaya na homoni za mwili zinakuwa katika mpangilio usioendana; wanaume kwa wanawake.

MATIBABU YAKE

Matibabu ya kupunguza uzito uliopindukia ili urudi wa kawaida huambatana, unaanzia na kuboresha mazoezi ya mwili.

Pia, kuna suala la kuimarisha ubora wa chakula mtu anavyotumia, kwa kadri inavyoshauriwa kitaalamu kwa mhusika.

Kuna dawa maalumu za kukabiliana na unene, zinazotumiwa kupunguza hamu ya chakula au kuzuia ufyonzaji mafuta mwilini.

Upande wa unene tumboni, kuna mpira mpira maalumu wa kufunga tumboni unaosaidia kupunguza uzito wa mwili.

Kuna wakati inaopibidi, kuna upasuaji maalum wa mwili hufanywa kupunguza ama ukubwa au urefu wa tumbo au vyote kwa pamoja.

Daima upasuaji huo unalenga kuujenga mwili wa mtu kushiba upesi na kupunguza uwezo wa mwili huo kufyonza virutubishi vilivyomo katika chakula.

Wataalamu wa chakula na lishe wanashauri watu wazidi kufanya mazoezi, kula vyakula kulingana na kundi lao la damu na aina ya vyakula unavyopaswa kuliwa, ili kupunguza uzito wa miili yao,

Columnist: www.tanzaniaweb.live