Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

NIONAVYO: Hatua ya makundi CAF itasisimua Dar

Simba Rekodi CAF Wachezaji wa Simba SC

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) juma hili lilitoa ratiba ya hatua ya makundi katika mashindano ya klabu kwa upande wa Ligi ya Mabingwa (Caf Champions’ League) na Kombe la Shirikisho (Caf Confederation Cup).

Klabu za Simba na Yanga zinashiriki mashindano haya. Simba iko kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa huku Yanga ikiwa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hizi kushiriki hatua ya makundi kwa wakati mmoja.

Mashindano haya yatafanyika kuanzia Februari hadi Aprili mwakani huku klabu za Yanga na Simba zikithibitisha kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani.

Simba iliyo katika kundi C la mashindano ya Ligi ya Mabingwa imepangwa pamoja na timu za Raja Cassablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea na Vipers FC ya Uganda. Yanga iliyo katika kundi D la mashindano ya Shirikisho imepangwa pamoja na timu za TP Mazembe ya Congo DR, US Monastir ya Tunisia na AS Real Bamako ya nchini Mali. Hiyo inahakikisha kuwa kuna michezo sita ya klabu barani Afrika itakayochezwa katika kipindi cha miezi miwili ndani ya Dar es Salaam.

Dar itapokea wageni kutoka Morocco, Guinea, Uganda, Kongo DR, Tunisia na kwingineko.

Hii ni nafasi kwa wapenzi wa mpira wa miguu wa Dar es Salaam na mikoani kufurika ëKwa Mkapaí kujipatia furaha lakini pia wafanyabiashara ya hoteli na huduma nyinginezo hii ni fursa kwao. Kutokana na kuwepo kwa klabu zinazotokea nchi za jirani, yaani TP Mazembe ya Elizabethville (Lubumbashi), Kongo DR na Vipers ya Kampala, Uganda kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo wageni wa ziada kutokana na makundi ya mashabiki yanayoweza kusafiri kwa njia mbalimbali kuja Dar.

Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla imesifika kwa kuwa na mashabiki wengi wanaokuja kushangilia timu zao zinapocheza nyumbani. Sifa hii ilijidhihirisha hasa kipindi ambacho dunia ilikuwa ikipambana na ugonjwa wa Covid 19 huku viwanja vingi duniani vikijikuta na mashabiki wachache au bila mashabiki lakini bado michezo kwenye viwanja vya Tanzania ilijaza umati mkubwa wa mashabiki.

Muda wa maandalizi ni sasa. Mpira uko upande wa Simba na Yanga kuziandaa timu zao hili ziweze kufanya vizuri katika mashindano hayo ili ziendelee kuungwa mkono katika mashindano haya na yajayo. Kwa kadri timu za nyumbani zinavyofanya vizuri ndivyo mzuka wa mashabiki kufurika kuzishuhudia timu zao unavyozidi kupanda. Kila la kheri Simba Sports Club, kila la kheri Young Africans SC.

Columnist: Mwanaspoti