Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

NGUMI: MAGUFULI AMETUACHIA ULINGO

567bccaa5390099172f82f7caa24d934.png NGUMI: MAGUFULI AMETUACHIA ULINGO

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limesema litaendelea kumkumbuka Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli kwa mabadiliko aliyoyafanya katika mchezo huo, lakini kubwa ni kitendo cha kuwasaidia kupata ulingo.

BFT ambao kwa muda mrefu kilio chao kilikuwa ni ulingo kwa ajili ya mazoezi pamoja na mashindano mbalimbali ya vijana, ambapo Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kuzumngumza na serikali ya China ambayo ilikubali ombi hilo.

Ofisa habari wa shirikisho hilo, Potipoti Yusufu alisema jana kuwa, licha ya Rais Magufuli kuwasaidia kupata ulingo, lakini pia alikuwa msaada kwa kuwapa nafasi vijana wenye uwezo kujiunga na majeshi kwa ajili ya kuundeleza mchezo huo.

“Sisi kama shirikisho tumepoteza mtu muhimu ambaye alitusaidia kwa mambo mengi ametuachia alama ambayo haitafutika kirahisi,” alisema.

Yusufu alisema pia anamshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa nafasi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa na naibu wake, Abdallah Ulega ambao wameleta chachu katika michezo hasa ngumi ambao ulikuwa umepoteza mvuto.

Columnist: www.habarileo.co.tz