Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mwamuzi Komba alipotufundisha somo la VAR Simba vs Ihefu

Mwamuzi Komba Pic Data Mwamuzi Komba alipotufundisha somo la VAR Simba vs Ihefu

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kama timu kongwe nchini, Simba ingetoka suluhu na Ihefu, Jumamosi ya Novemba 12 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, basi Mwamuzi Msaidizi wa kimataifa wa Tanzania, Frank Komba angekuwa mpaka sasa ananangwa sana na wadau wa soka. Naweza kusema kuwa mchezaji Pape Ousmane Pape ndiye aliyesababisha kutokuwepo kwa shutuma nyingi kwenye mitandano ya kijamii kwa kufunga bao katika dakika ya 62 na kuifanya Simba kuibuka na ushindi.

Komba ambaye Januari mwaka huu alichezesha michuano ya AFCON nchini Camaroon, alitufundisha kwa dakika chache umuhimu wa Teknolojia ya Mwamuzi Msaidizi wa Video (VAR) katika mchezo huo ambao ulichezeshwa na mwamuzi mzoefu Nassoro Mwinchui.

Waamuzi wengine katika mechi hiyo walikuwa Ephron Ndissan ambapo mwamuzi wa akiba alikuwa Shafoo Mohamed.

Komba alituingiza darasani katika dakika ya 20 ya mchezo huo kwa kuwasiliana na mwamuzi wa kati, Mwinchui kuwa Habib Kyombo alifanyiwa faulo na mchezaji wa Ihefu akiwa nje ya eneo la penalti.

Awali, Mwamuzi Mwinchui alionyesha ishara ya kuwa faulo aliyofanyiwa Kyombo ni penalti na kusababisha wachezaji wa Ihefu kumzonga kwa dakika kadhaa. Wakati wa mabishano hayo, Komba aliwasililiana ki-VAR na Mwinchui na kusisitiza kuwa faulo hiyo ilikuwa nje ya eneo la penalti na mwamuzi huyo kufuata.

Nimesema kuwa kama Simba isingeshinda mchezo huo, basi wadau wa soka wangekuwa wana wanawasimanga waamuzi hao na maneno mengi yangekuwa yamesemwa mpaka sasa.

Hii ndiyo ‘mila na desturi’ ya mashabiki wa soka na ‘watu wa mpira’ ambapo kwenye zuri, basi pongezi (appreciation) huwa ni vigumu kupewa mtu aliyefanya jambo hilo.

Ni wazi kuwa jambo baya linazungumzwa sana kuliko zuri na ndiyo maana jambo zuri la Mwamuzi Msaidizi, Frank Komba hajapongezwa mpaka sasa na mitandao ya kijamii imekuwa kimya sana.

Pamoja na Komba kufanya kazi yake ipasavyo, nichukue fursa hii kumpongeza kwa jambo hilo kwani ndiyo msingi mkuu wa kolamu hii ya VAR. Kazi kubwa ya kolamu hii ni kuelimisha ndiyo maana kwenye upungufu tunatolea ufafanuzi na kwenye mazuri pia tunapongeza ili kuhamasisha wengine kufanya vyema zaidi ya aliyepongezwa.

SOMO KUTOKA KWA KOMBA

Kwanza Mwamuzi Msaidizi Komba amethibitisha ubora wake ambapo umesababisha CAF kumchagua kuwa miongozi mwa waamuzi waliochezesha michuano ya AFCON nchini Cameroon.

Komba ametufundisha kazi halisi ya mwamuzi msaidizi katika soka. Kuna usemi kuwa mwamuzi wa kati akitoa maamuzi, basi hayawezi kubadilishwa… Ni msemo ambao wadau wa soka wamezoea kuusikia na kuna baadhi ya waamuzi wakifanya hivyo basi husimamia maamuzi yao hayo hayo.

Moja ya maeneo yenye matatizo makubwa katika soka ni sheria namba 11 ya kuzidi au kuotea na sheria namba 12 ya makosa na nidhamu mbaya.

Mwamuzi msaidizi mara nyingi huzingatia mpira kutoka na kuzidi na mara nyingine faulo ambazo zinatokea katika eneo ambalo yeye yupo karibu.

Katika suala la kuzidi, mwamuzi msaidizi humzingatia zaidi beki au mchezaji wa mwisho wa timu inayozuia (defend) na kuwa sawasawa naye. Kwa suala la Kyombo, Komba alifaulu kwa kiasi kikubwa kwa kukimbia sambamba na mshambuliaji huyo mpaka baada ya kufanyiwa faulo. Hivyo alikuwa ‘fit’ kumudu kasi ya wachezaji wa ndani.

Kama angekuwa hana ‘fitness’, hasingeweza kuona sawaswa tukio zima na maamuzi yangekuwa tofauti.

Pili, umuhimu wa VAR umeonekana kupitia mechi hiyo ya Simba na Ihefuu. Mwamuzi Komba ameonyesha wakati tunasubiri ‘kuwekewa’ VAR katika siku za usoni, waamuzi wanaweza kujiridhisha kwa kuwasiliana ili kupata maamuzi sahihi katika michezo mbalimbali na kuondoa malalamiko na kuboresha zaidi ligi yetu.

Columnist: Mwanaspoti