Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mtazamo wa Mkapa kama Gorbachev wa Urusi

45fbdb400fc16812baa09c623841bbfd Mtazamo wa Mkapa kama Gorbachev wa Urusi

Mon, 27 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATANZANIA wemekumbwa na pigo kwa kuondokewa na Rais wa awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hatua iliyowakumbusha machungu ya mwaka 1999 walipoondokewa na Rais wao wa kwanza, Mwalimu Julius Nyerere. Rais Mkapa alipoingia madarakanai, aliweka wazi kwamba utawala wake ungeheshimu uwazi na ukweli kwa maana ya kwamba Tanzania ilikuwa imeingia katika zama za kutoficha mambo.

Ingawa falsafa ya utawala wa sasa chini ya Rais John Magufuli ni ‘Hapa Kazi’ tu lakini umekuwa pia ukienzi kwa kiasi kikubwa mtazamo huo uwazi na ukweli wa Rais Mkapa.

Rais Magufuli amekuwa mkweli pengine unaweza kusema kupita kiasi huku akitumia maneno; ‘Msema kweli ni mpenzi wa Mungu” au ‘tunamaliza hapa hapa’.

Magufuli aliyeibuliwa na Mkapa mwaka 1995 kwa kumpa unaibu waziri ambao aliutendea haki, amekwenda mbalimbali zaidi hadi kuondoa usiri hata katika kuwapata wagombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Hata hivyo, kumbukumbu zilizopo zinaonesha kwamba mwasisi wa siasa zinazozingatia ukweli na uwazi duniani ni aliyekuwa Rais wa Urusi, Mikhail Gorbachev aliyeingia madarakani na kauli mbiu ya “Glasnot” neno la Kirusi linalomaanisha ukweli na uwazi.

Gorbachev alikuwa na kauli nyingine ya “Perestroika” ambayo maana yake ni mwanzo mpya. Mkapa alipoingia madarakani, aliikuta nchi ikiwa imetawaliwa na dhana ya ruksa ya utawala wa mtangulizi wake, Mzee Ali Hassan Mwinyi, iliyosaduifu hatua ya serikali kuja na siasa za uliberali baada ya miongo takribani miwili ya kujaribu kujenga ujamaa.

Dhana ya ruksa ulitokana na nguvu za nchi za magharibi zilizozitaka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kujielekeza katika mfumo wa marekebisho ya uchumi ulioongozwa taasisi za fedha za kimataifa; Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya dunia (WB).

Kutokana na siasa hizo kuiruhusu nchi kukopa kwa masharti ya kuruhusu soko huria, Mkapa aliikuta Tanzania ikidaiwa madeni mengi na taasisi za ndani na nje, yakiwemo madeni ambayo yalirithiwa tangu wakati wa serikali ya awamu ya kwanza.

Alikuta pia hali ya viwanda vingi vilivyoanzishwa na serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ikiwa mbaya baada ya kuumizwa na ushindani uliotokena na soko huria sambamna na ubadhirifu, viwanda vingi vikiwa havifanyi kazi.

Mkapa akaamua kubinafsisha viwanda ili visiendelee kuwa mzigo kwa serikali na pengine vikafufuka na kuongeza ajira nje ya mfumo wa umma.

Kama Gorbachev alivyoikuta Jamhuri ya Kisoviet ya Uruisi ikiwa katika hali mbaya ya kiuchumi, Rais Mkapa pia alikuta bei za badhaa zikipaa kila siku, hali iliyosababisha pia shilingi yetu kushuka thamani kwa haraka.

Hadhi ya baadhi za kazi katika sekta ya umma ilishuka sana kutokana na watu wengi kukimbilia katika biashara ili kujiingiza pesa haraka haraka kwa kuuza bidhaa mbalimbali hata kupitia njia za ulanguzi, magendo na rushwa.

Kazi kama ualimu ulidharauliwa na wengi na hivyo Watanzania wengi kukimbia kazi hiyo ambayo zama za Mwalimu Nyerere iliheshimika sana. Hatua hiyo kwa kiasi kikubwa ilichangia hali ya elimu nchini pia kushuka.

Kwa nini Gorbachev alitaka kuibadilisha Urusi kupitia kauli mbiu zake za ukweli na uwezo na mwanzo mpya?

Aligundua kuwa silaha za nyuklia za Urusi zisingeweza kushindana na silaha za nyuklia za Marekani, ambayo ilikuwa na uwezo wa kumiliki na kutengeneza silaha zaidi kuliko Urusi.

Hivyo aliamini katika kuelezana ukweli, kushirikiana na Marekani badala ya kuendeleza vita baridi. Alitangaza kuacha kutumia fedha kwenye silaha za maangamizi na miaka miwili baadaye, Marekani na Urusi walitia saini mkataba wa kuondoa silaha zao nchi za Ulaya na wakati huo huo Gorbachev alianzisha uhusiano mzuri kati ya Urusi na dunia nzima.

Aliondoa majeshi ya Urusi kutoka Afghanistan ambako ilikuwa ngomne yake kubwa.

Kwenye risala zake, Mikhail Gorbachev ambaye alikuwa mahiri sana katika kuandaa hotuba kama alivyokuwa Mkapa aliongelea ushirikiano na uaminifu wa kimataifa dhidi ya Urusi.

Gorbachev alipendwa na watu Mtazamo wa Mkapa kama Gorbachev wa Urusi lakini sera zake hazikufanikiwa sana kama alivyotegemea.

Baada ya miaka miwili ya sera za Glasnot na Perestroika, ilikuwa wazi, kuwa uchumi wa USSR usingeweza kutengemaa haraka kama watu walivyotaka. Hata hivyo, Gorbachev aliendelea kutoa mijadala ya wazi kuhusu sera za Serikali na ukweli sehemu mbalimbali ndani na nje ya Muungano wa Soviet ili kuweza kukabiliana na matatizo mbalimbali yaliyokuwa yanalikabili taifa lake.

Mnamo mwaka 1987 program ya Perestroika iliweza kuleta sera mpya za soko huria kwa lengo la kunusuru Uchumi wa Taifa hilo kubwa duniani. Mkapa pia wakati wa utawala wake aliendelea kulipa madeni yaliyokuwa yakiikabili nchi hadi wakati fulani kuitwa ‘mlipa madeni’ huku pia akiendelea na ubinafsishaji wa mashika ya umma yaliyoonekana mzigo.

Swali ni je, ubinfasaji ulileta manufaa yoyote? Katika kujibu swali hilo, hata Mkapa mwenyewe katika kitabu cha maisha yake cha My Life, My Purpose anakiri kwamba ingawa nia ilikuwa njema sana lakini ubinafsishaji haukuleta manufaa makubwa kwa taifa kama ilivyotazamiwana na kwamba udhaifu ulikuwa ni kutoweka usimamizi thabiti.

Hali ya sintofahamu ya kuanguka kwa mashirika ya umma yakiwemo yaliyoingia ubia na serikali iliendelea kuwa kama alivyoiacha Mkapa hadi alipoingia madarakani Rais John Magufuli ambaye katika sera yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda mashirika haya yameangaliwa upya ili yatimize malengo yaliyokusudiwa wakati yanaundwa.

Rais Mkapa kupitia baraza lake la mawazili aliloliita askari wa miamvuli, atakumbukwa pia kwa jinsi alivyojitahidi kudhibiti mfumuko wa bei.

Takwimu zinaonesha kwamba wakati akiingia madarakani mfumuko wa bei, tatizo linalokabili nchi nyingi duniani ulifikia zaidi ya tarakimu mbili lakini katika uongozi wake aliupunguza kwa kasi hadi kusomeka tarakimu moja.

Bwana alitoa, na bwana ametwa. Jina la bwana limidiwe.

Columnist: habarileo.co.tz