Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Msuguano mkali Marekani, China nani ashike mamlaka Benki Afrika

USVSCHINA Msuguano mkali Marekani, China nani ashike mamlaka Benki Afrika

Fri, 26 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Iimeshindikana kumng’oa Mkurugenzi Marekani kususa? Kicheko kwa Mchina

MABADILIKO makubwa katika safu ya wanahisa yanatazamiwa kushuhudiwa katika wiki kadhaa zijazo, kutokana na tofauti za kubwa zilizopo kati ya serikali ya Marekani na Rais wa Benki ya Maendeleoo ya Afrika (AfDB), Dk. Akinwumi Adesina.

Marekani imeshindwa kuishawishi bodi ya benki hiyo kumchunguza kwa undani Rais wa AfDB na imekuwa ikieleza kutokuwa na imani na sera anazozifuata, licha ya wanahisa wengine na hasa mwanahisa wa kwanza Nigeria, anakozaliwa Rais wa sasa wa AfDB, anayeeleza kuridhishwa na utendaji wake.

Wachambuzi wa habari wanasema, Marekani haitafunika aibu ya kukwama, ila itajitoa.

Suala hilo lilifikia kilele chake mwanzo wa mwezi Juni. wakati bodi ya AfDB ilipoungana na Kamati ya Maadili ya benki hiyo, iliyofanya uchunguzi kuhusu tuhuma za Marekani, dhidi ya Adesina na kuzitupilia mbali hoja zote.

RERCORD

Ni hoja zilizowasilishwa katika bodi hiyo kwa kutumia barua ya Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, aliyetoa madai yanayofahamika na kuorodheshwa, kisha kupigiwa debe na Stephen Dowd, Mjumbe wa Marekani katika Bodi ya AfDB,

Kunatamkwa kuwapo malalamishi kadhaa ikiwemo upendeleo katika uteuzi wa kujaza nafasi katika benki hiyo na kutumia benki kama chombo cha kisiasa, kujipigia debe arudi madarakani, wakati wanahisa wakimchagua rais wa benki hiyo kwa miaka mitano ijayo, mwezi Agosti ijayo.

Marekani imshahangaikia kuondolewa kwa Dk Adesina, ikashindikana kutokana na wadau wengine kutolikubalia, halafu inapinga kwa nguvu mshindani wake China katika shughuli za benki hiyo, hasa katika kuundwa mfuko wa uwekezaji unaoitwa Jukwaa la Uwekezaji Afrika (AIF).

Hadi kufika mwisho wa mwaka jana, kulishawekezwa Dola za Marekani bilioni 80 fedha zilizoelekezwa katika miundombinu, mwelekeo unaopingwa na Marekani,

Nchi hiyo inadai hatua hiyo ya AfDB, imekiuka mpangilio wa majukumu iliyopewa kutekeleza. Hata hivyo, wanahisa wengine walipongeza hatua hiyo.

Wachambuzi wanasema, kutokana na tofautii hizo, haitawezekana kwa Marekani kuendelea kuwa mwanahisa na Mjumbe wa Bodi ya AfDB, hatua iliyochukua sura katika Shirika la Afya Duniani (WHO).

CHINA VS MAREKANI

Mwaka jana, Mmarekani huyo Mjumbe wa Bodi ya AfDB, Dowd, aliandika makala ya maoni katika gazeti moja nchini kwao, akieleza masikitiko yake kuwa Adesina, hajaonyesha kujali namna China inavyokuwa na nguvu kubwa katika uchumi wa nchi nyingi za Afrika.

Pia, anaeleza kutoridhishwa kwa Marekani kukosa kura ya veto katika shughuli za benki hiyo ya Afrika, wakati ni mwanahisa wa nne kwa ukubwa, nyuma ya Nigeria, Misri na Ujerumani.

Inavyoelekea, Uamuzi unaochukuliwa na bodi kukubaliana kwa pamoja kisha inapigwa kura, ni hali ambayo Marekani katika mtazamo wa kawaida, ilipaswa iungwe mkono kimtazamo na Ujerumani, kwa mfano AfDB isiwe mwenyeji wa jukwaa hilo.

Anasema, katika uchambuzi huo, msimamo wa Adesina hakuna haja ya kuhangaika na uwepo wa China na nguvu kubwa katika uchumi wa Afrika.

Pia, kutokuwepo Marekani katika nguvu hiyo, unaikera sana nchi hiyo, hata kufikia hatua ya kuunda mifumo mingine ya kimataifa ya kuingiza fedha katika maendeleo ya Afrika, yenye uwezo wa kushindana na AfDB, pamoja na Jukwaa la Uwekezaji.

Ikirejewa mwaka jana, Marekani iliunda kinachopitwa DFC (Development Finance Corporation) kwa mtaji wa Dola za Mareakni bilioni 60.

Baadhi ya wachambuzi wanasema, Marekani ina nguvu kubwa katika Benki ya Dunia, hivyo ikiunganishwa na DFC, itakuwa na nguvu kubnwa zaidi, hoja inayopingwa na baadhi ya wachambuzi.

Marekani inamteua rais wa Benki ya Dunia, lakini sera zake ni tofauti. Baadhi ya wachambuzi nchini Nigeria, wanasema hadi kufikia mwezi uliopita nchi hiyo ilishafikia tamati na itatumia kutoridhishwa kwake na majibu ya Kamati ya Maadili ya Bodi ya AfDB na huenda ni sababu ya kujitoa.

Wako wanaosema, ni hali itakayoiweka shakani AfDB kwa kupungukiwa na mtaji, suala ambalo baadhi ya wadadisi hawaoni umuhimu wake.

Tayari mtaji uliopatikana kutokana na Jukwaa la Uwekezaji utakuwa unazidi wa Marekani katika benki hiyo na kama China hivi sasa siyo mshirika muhimu na bodi inaweza kupitisha kuchukuliwa nafasi kubwa zaidi, kama haitaongeza mtaji wake kufikia iliposimama Marekani.

Suala hilo limeteka hisia za wachangiaji kwenye mtandao wa gazeti la Guardian nchini Nigeria, ambako kuna maumivu kuhusu Marekani, hasa jinsi ilivyomzuia Waziri wa Fedha wa zamani nchini humo, Dk. Ngozi Okonjo-Iweala, kupewa nafasi ya Rais wa Benki ya Dunia.

Mchumi huyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Standard Chartered nchini Uingereza, hivi sasa ni Balozi Maalum anayekusanya misaada kwa Shirika la Kimataifa la Chanjo, kusaidia bara hilo na kupambana na ugonjwa corona.

Nafasi ya Rais wa Benki ya Dunia, aliyokuwa anaitaka raia huyo wa Nigeria, ilishachukuliwa na David Malpass, Naibu Waziri wa Fedha nchini Marekani na ameshiriki kwa miaka mingi kuunda sera Marekani hasa kuhusu madeni nchi zinazoendelea.

Mkasa huu kuhusu Adesina ni mwendelezo wa kutokuelewana kati ya utawala wa Rais Donald Trump nchini Marekani na taasisi kadhaa za kimataifa, na uhusiano wa taasisi hizo na China kila mara unakuwa ni suala la msingi.

Tatizo lililopo sasa ni kwamba, China inataka kuchukua nafasi yake katika uchumi wa kimataifa, pasipo kuwekewa vipingamizi, wakati haifungui milango ya kununua hisa katika mashirika ya umma na benki.

Pia, nchi kama Marekani hadi sasa haina taasisi kama hizo, ila mashirika ya kuratibu sekta tofauti. Inaeleza nguvu za kiuchumi za kampuni za China zinazopata mtaji wowote inazohitaji kutoka serikali ya China, inavuruga ushindani katika kutafuta tenda tofauti nchi nyingi duniani, kwa kutoa bei ya chini kwa kandarasi za ujenzi.

Columnist: www.tanzaniaweb.live